Dar es Salaam
Ili kusadifu ukuaji wa sekta ya Ujenzi na majengo yanayoendana na ukuaji wa kasiwa teknolojia ya ujenzi,Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuwaamini Wakandarasi wa Ndani kwa Miradi Mbalimbali ikiwemo ile mikubwa ambayo wanaweza wakafanya vizuri kwani Serikali tayari imeongeza wigo mpana katika sheria ya manunuzi kwa lengo la kuwanufaisha Wazawa.
Hayo yamesemwa na naibu waziri,wizara ya Ujenzi Mhandishi Godfray Kasekenya wakati wa Ugawaji wa Tuzo za Ujenzi na Majengo Afrika Mashariki kwa Mwaka 2023 (EABC), zilizofanyika Katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam usiku wa Disemba 5,2023
Mhandisi Kasekenya amesema wahandisi wanapaswa wapate vifaa bora ikiwemo Saruji, nondo, misumari, vigae, marumaru na bidhaa zote zinazotumika kwenye ujenzi ambazo zinazalishwa na kampuni hizo.
“Ukiwa mhandisi mzuri halafu ukapata bidhaa zisizobora basi hautafanya chochote kizuri. Moja ya kitu ambacho Serikali tunakitaka ni kuwa na vifaa na uhandisi bora hivyo tunatoa wito kwa wadau wanaojihusisha eneo hili kutoa huduma zilizobora ambazo zinaingia kwenye mnyororo mzima wa ujenzi”, amesema Mhandisi Kasekenya
Hata hivyo Mhandisi Kasekenya amewataka wajenzi na watoa huduma za ujenzi kufanya kazi kwa uadilifu na kwa kushirikiana na serikali huku akitoa rai kwa Watanzania kuzidi kuwatumia wataalamu wa ujenzi pindi wanapokuwa na miradi ili kuwa na uhakiki na usalama wa miradi yao kumalizika kwa wakati na kuwa bora.
“Usipowatumia wataalamu ujue mbele ya safari inawezekana ukapata hasara. Kama unajenga nyumba hakikisha imesanifiwa na mtaalamu hata asipojenga yeye hakikisha anakupa ushauri”, amesisitiza Naibu Waziri huyo.
Tuzo za Ujenzi na Majengo za Afrika Mashariki kwa Mwaka 2023 umeshindanisha makampuni zaidi ya 500 kwa lengo la kuongeza ushindani miongoni mwa wadau wa Sekta ya Ujenzi, lakini pia kufanya chachu ya utoaji wa huduma bora katika mnyororo mzima wa Sekta ya Ujenzi.
Kwa upande wake Mratibu wa tuzo hizo Steven amesema kuwa wameamua kuandaa tuzo hizo ili kusaidia kukuza sekta ya ujenzi hapa nchini pamoja na wabunifu katika sekta ya majengo
Mratibu huyo amesema kuwa tuzo hizo si tuu zitakuza heshima ya ujenzi na majengo Afrika Mashariki bali zitasaidia kuwatangaza Afrika Mashariki.
Nao baadhi ya makampuni yaliyoshinda tuzo hizo akiwemo Angela Maingu kutoka kampuni ya Modern Industrial park amesema tuzo hizo zitawajngea imani kwa wateja wao na zimewapa hari ya kufanya kazi kwa bidii huku akiishikuru serikali kwa kuithamini sekta ya ujenzi na majengo.
0 Comments