TAASISI YA MAMA ONGEA NA MWANAO IMETOA VITI 250 KWA WATOTO WALEMAVU.

 


Na Mwandishi  wetu

Taasisi. ya Mama Ongea na Mwanao  kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wametoa msaada wa viti mwendo 250 kwa watoto wenye mahitaji maalumu (Walemavu) ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao za kupata elimu .


Hayo  yamesemwa.  jijini Dar es Salaam na  Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Steve Nyerere amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakipitia wakati mgumu mara baada ya kujifungua watoto wa aina hiyo kwani wanaume huwatelekeza  wake zao.


"Baadhi. Ya wanaume  ni wazembe katika kulea Watoto wenye Ulemavu hufikia kuwa kana kuwa mtoto mwenye Ulemavu si wake, lakini mtoto akiwa na hana ulemavu anamdai mwanamke kuwa mtoto ni wake," amesema Nyerere.


"Sisi  kama  taasisi  ya mama ongea na mwanao tunatakiwa   kupeleka Mahitaji  kwa Wenye uhitaji popote walipo hivyo tunaomba taasisi nyingine zituunge mkono," amesisitiza Steve Nyerere.


Naye  Katibu wa Taasisi Ongea na mwanao Evon Sherry amesema taasisi hiyo imetembelea mikoa mitano na kubakisha mikoa miwili 


"Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anawasaidia wakina mama katika sekta ya Afya,Maji lakini Sisi tumeamua kumtua mama mtoto mgongoni" amesema Evon.

Post a Comment

0 Comments