DC KUBECHA AAGIZA KUKAMILIKA KWA UJENZI WA MAABARA KATIKA SHULE YA SEKONDARI KIRARE

 






Mkuu wa Wilaya ya Tanga Leo Tarehe 16 Mwezi 4,2025 Amefanya ziara ya kushtukiza katika muendelezo wa Ziara zake za kukagua maendeleo ya miradi na Huduma katika wilaya ya Tanga.

Katika ziara yake aliyoifanya katika shule ya Sekondari Kirare alijionea changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kutokamilika kwa wakati kwa Miradi ya Maabara mbili na Nyumba ya waalimu ambazo zilipaswa kukamilika toka mwezi November mwaka Jana,

Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Japhari Kubecha ameagiza Kukamilika kwa miradi hiyo kwa muda wa Mwezi mmoja kuanzia Leo,Huku akitoa maelekezo ya kuondolewa kwa Fundi aliyeshindwa kukamilisha mradi huku akiwa amelipwa fedha za Mradi.

Post a Comment

0 Comments