Katibu wa Machinga Dar Masoud Aimwagia Sifa Serikali

 

Na: Francis Peter

Uongozi wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam kupitia kwa katibu wake Masoud Chauka umesifia  hatua kubwa inayofanywa na  Serikali nchini inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mikakati yake ya kuendelea kutengeneza mazingira ya kutengeneza faida kwa machinga .



Akizungumzia Dar es Salaam  juu ya juhudi za serikali kwa sasa, Masoud amesema Uongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) umekuwa imara kuwapa mrejesho sahihi viongozi wake hivyo tumekuwa na hatua nzuri ya kuelekea mafanikio.

"Nikiwa kama katibu wa mkoa huu , hivi karibuni nimeshiriki kikao na baadhi ya benkihapa nchini na hali inaonesha kuja kuwa na muonekano mkubwa wa kimafanikio kwani serikali imekuwa ikitaja kutujengea mazingira rafiki kwa kuweza kutufanyia wepesi wakujikwamua kwa kupata mikopo,"alisema Masoud.

Ameitaja NMB kuwa ni moja ya benki iliyoweza kukubali kutaka kutoa mikopo katika maongezi yao hali ambayo itachochea maendeleo yao ya kukuza mitaji .



"Ni hatua nzuri kuwa benki ya NMB itaweza kutoa mikopo midogo midogo kuanzia Mil 3 kwa wamachinga waliokatika maeneo yao sahihi ambapo ambapo wenye vizimba vyao watapatamikopo hadi wa shilingi Mil 5 ,"amesema.

Kiongozi huyo ameipatia sifa serikali ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwaangazia fursa hiyo katika biashara zao jumuishi kwani, fursa hiyo imelenga kukuza uchumi  jumuishi kwa wamachinga.



Post a Comment

0 Comments