BINTI NI NGUZO NA KIOO KATIKA JAMII

 









Hayo alisyasema  jana Dkt. Gladness Salema alipokuwa anazindua kitabu kinachoitwa BINTI KAMA NGUZO ambacho kimeandikwa na Dkt Kanuti,ambapo alisema kuwa 

" Huyu binti anaitwa binti kama Nguzo,ukisema kuna kitu ni nguzo maana yake kina uwezo wa kubeba uzito na kwa hiyo ukiambiwa wewe binti ni nguzo,nakuomba ufikiri Mara mbili"


"Vigezo vyake havishikiki kwenye hii nguzo,kuna mchanga,kuna cement na  Ili uitwe nguzo tunaongelea uwezo,yaani ya Dunia ni mazito,hata hizo ndoa mnazotaka ni zito"


Na aliongelea maisha ya wanavyuo wa vyuo  vikuu kwamba washikilie kitu kimoja kwanza na wasiwe na haraka na maisha ambapo alisema kuwa  "Yaani pale chuo first year ananiuliza habari ya uchumba,huwa nashangaa wataweza kuwa nguzo!!!??


" Hapo ulipo na fomrsix yako utaweza kulea watoto,Bado unatengeneza kokoto bado unasuka suka vinondo vyako utaweza kuwa nguzo,wenzio wanazunguma Ndoa wewe zungumza GPA"


"Ili uweze kubeba uzito wowote kwenye maisha yako unatakiwa Kuwa Nguzo kwenye Maisha yako"


"Ili uwe Nguzo ni suala la uwezo,nguzo ni kuhusu uwezo wa kubeba vitu kwa wakati,ukisoma 2Timotheo4:7"


"Ili uitwe nguzo lazima uwe kwenye battle filled,hapa Duniani lazima ujue unapoelekea,Binti nguzo hawezi kuwa mpumbavu anajua anapoelekea,hata kama yuko kwenye misukosuko huwa anapambana kwenye maisha yake"


"Pia alizungumzia kuhusu maono hususa ni kwa mtoto wa kike ambapo alisema kuwa (kusambaa kuna gharama, simamia kile ulichonacho,je mnapigana vita sahihi kwa majira sahihi"


"Lazima ujue unapoelekea na vita yako iende pale unapoelekea,muwe na kituo kwamba Nipo hapa nahatamia au natafuta hiki"


"Nguzo inabeba majukumu,baki hapo kwenye battle filled uweze kufika na muwe na Speed ya uthubutu,speed ya utekelezaji,there is a race that we must win"


"Duniani there is a race,there is competition,you must be competitive, Duniani kuna ushindani"


Pia aliongelea kuhusu Nidhamu na katika kujenga Nguzo ambapo alisema kuwa "Commitment, Displine,kubali kujenga hata leo hapa umejengwa na ukishajengwa tutachongwa"


"Sasa nguzo haipo tunachonga nini,lazima uwe na nidhamu ili ujenge nguzo"


Na alihitimisha kwa kusema kuwa "Kwa mwanamke lile eneo that is your Price, hata kama unamaakili,unamapesa lakini wale jamaa wanajua.,wewe nani usijaribiwe,hata uolewe utajaribiwa,sasa wewe nani usijaribiwe??


Na aliongezea kusema umuhimu wa muda kwenye maisha ambapo alisema kuwa ""Tofauti yetu ipo ndani ya masaa 24,kuanzia leo unapotoka hapa,unaenda kuishije unaenda kufanya nini"

"Hulipii masaa 24,Fanya Yale ambao yanaendana na na wewe mwenyewe,

Kwa hiyo masaa 24 ni Rasimali ambayo Mungu ametupa Bure"



"Kristo ni kristo,wokovu ni wokovu, weka nguzo ya uchapakazi,weka nguzo ya kutengenezeka,kwenye kujengwa,lazima wewe mwenyewe uwekeze"


"Kama unataka kuchonga kachonge maisha yako,hakuna maombi ya kukuchonga,kajichonge na kajitengeneze mwenyewe"


Naye  Mwandishi Na Mkufunzi Kutoka chuo cha Ardhi,Dkt.Arbogasti Kanuti. Alisema kwamba  ambaye ameandika  kitabu cha BINTI KAMA NGUZO  alisema kuwa "kitabu hiki ni sauti kutoka ndani ya moyo wangu,ni kilio cha mabinti wengi,na nilikiandika kitabu hichi nikichora picha ya binti mwenye ndoto,ambaye anatafuta thamani yake katika jamii"


"Mabinti thamani yenu ni kubwa sana na jamii imewadogodehsa sana,na na Natangaza kwa ujasiri kwamba Binti ni nguzo"


"Binti akielekezwa akijatambua,anaweza kuwa taa katika kizazi hiki cha Giza na kuwakomboa wengine"


"Binti jitambue kama wewe ni wa thamani,jifunze na jijenge na jitambue kwamba utafika mbali"


"Na ni miongozo kwa wazazi na kwa walezi,waalimu na watu wote katika jamii, kwamba tunajukumu la kumjenga binti"


"Vilevile jamii Naomba iamini kwamba Binti anaweza kuwa Nguzo, hivyo naombeni mkisome kitabu hiki ili tuweze Kumkomboa Binti,katika kitabu hiki akili za mabinti zimefunguliwa na akili za mabinti zimewekwa wazi"

Alisema Kanuti.

Post a Comment

0 Comments