RC MAKALLA AAGIZA ANAOTUPA TAKA HOVYO KUANZA KUZOMEWA DAR

 



Na Teophil Mbunda

Kampuni ya WESE yenye dhumuni la kuwaletea manufaa Madereva wa vyombo vya moto vya biashara kwa kuwaletea mfumo wa kuwawezesha kukopa Mafuta bila riba wala kamisheni  wameendelea kushirikiana vyema na Serikali kupitia Madereva wa Daladala za Jiji la Dar es salaam kwa kuwapatia vifaa vya kuwekea taka  (Dustbin)  1000.


Akiongea Wakati wa  wa ugawaji wa Vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya WESE Bi Selina Masimba, amesema kuwa Kampuni hiyo  imekuwa na ushirikiano mzuri na Mabenki na Vituo vya Mafuta ambapo mpaka sasa imeshajiunga na Vituo vya Mafuta zaidi ya 50.



WESE yenye  Kauli Mbiu ya 'Tikisa Tenki, Piga bao' imekuwa na faida nyingi kwa Madereva kwa kuwainua Madereva kutoka kuendesha vyombo vinavyomilikiwa na watu na  kuwapa fursa ya kumiliki vyombo vyao vya Usafiri.


                                      Bi Selina Masimba Mkurugenzi wa Kampuni ya WESE

Akikabidhi Vifaa hivyo vilivyotolewa na Kampuni ya Wese Tikisa Tanki, Piga Bao, RC Makalla amesema Serikali kwa kushirikiana na Wadau wamefanikiwa kugawa Vifaa vya kuhifadhi taka kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo ili kuhakikisha Wananchi wanapata sehemu za kutupa taka.

Aidha RC Makalla ameelekeza Madereva na Utingo kuzitumia dustbin hizo kwa lengo lililokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuwakemea abiria watakaojaribu kutupa taka nje.





Pamoja na hayo RC Makalla amepongeza Kampuni ya Wese kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa huo kwenye suala la Usafi na kutoa wito kwa Wadau wengine kujitokeza.

Post a Comment

0 Comments