RIPOTI KAMILI YA AJALI YA NDEGE BUKOBA YAIBUA MAZITO





Ripoti ya Wizara kuhusu ajali ya ndege ya Precision imetoka. Baadhi ya mambo muhimu ni:
1. Bukoba airport haina control tower. Ndege zote zinazotua Bukoba marubani hujiongoza wenyewe.

2. Rubani alijua anatua kwenye runway wa uwanja, sio kwenye maji. Haikuwa water landing kama ilivyoelezwa na baadhi ya watu.
3. Kuna uwezekano ndege ilisukumwa na upepo (wind shear) kwenda ziwani, wakati rubani akijaribu kutua.
4. Landing gear haikua na tatizo na sio kweli kwamba tairi zilikataa kuchomoka kama ilivyoelezwa na baadhi ya watu.
5. Abiria hawakuwa na life vests/jackets.
6. Mlango ulifunguliwa na mhudumu mmoja wa ndege (wa kike) kwa kusaidiana na abiria mmoja (wa kiume) ndani ya ndege, na sio Majaliwa kama ilivyovumishwa. Abiria huyo ndiye aliyeshikilia mlango hadi watu wote wakatoka. Alipouachia ulijifunga na haukufunguka tena.
7. Kikosi cha polisi wa majini (Marine) kilikuwa nje ya Bukoba na kilifika masaa 4 baada ya ajali kutokea. Na hata kilipowasili, meli yao haikua na mafuta wala hawakua na mitungi ya oxgen, hivyo hawakuweza kufanya lolote.
8. Ukiondoa abiria wachache waliofariki papo hapo baada ya ndege kuanguka, abiria wengi walifariki kwa kuzidiwa maji, wakiwemo marubani wote wawili ambao hadi dakika 5 baada ya wavuvi kufika walikua hai. Juhudi za haraka zingefanyika abiria wengi waliofariki wangeweza kuokolewa.
9. Wavuvi hawakufungua mlango, bali walisaidiana kuwavusha abiria kutoka kwenye ndege kwenda ufukweni kwa kutumia mashua zao.
10. Kukosekana kwa control tower kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba (freequency 118.2MHz ) kunaweza kusababisha ajali mbaya ya ndege kugongana angani (mid air crash) ikiwa ndege nyingi zitatumia uwanja huo kwa wakati mmoja.!



Imeandikwa na Malisa GJ

Post a Comment

0 Comments