SHULE kongwe ya vipaji maalumu ya wavulana Kibaha Sekondari iliyopo Mkoa wa Pwani kwa Sasa inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu mkubwa wa majiko ya gesi kuvuja hali inahatarisha usalama maisha yawanafunzi pamoja na walimu kwani kunaweza kutokea mlipuko na kupelekea majanga ya moto.
Changamoto hizo zimebanishwa na mmoja wanafunzi wakati akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake katika halfa ya mahafali ya kidato cha nne ambayo yamehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wadau katika sekta ya elimu.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo hakusita kuweka bayana madhara ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na kuwepo kwa uchakavu huo na kuiomba serikali kuiangalia changamotoo hiyo kwa jicho la tatu.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ameahidi kushirikiana na serikali katika kuzitatua baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo.
Naye mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha akawaasa wanafunzi hao kuhakikisha wanapenda na kuthamini masomo yao ili kutimiza ndoto zao katika suala la elimu.
Shule hiyo kongwe ya wavulana Kibaha sekondari ni yawanafunzi wenye vipaji maalumu ambapo viongozi mbali mbali wa ngazi za juu walishawahi kusomea hapo akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete.
0 Comments