UVIKI WATEMBELEA MOI, WATOA MSAADA KWA WATOTO VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI









 Umoja wa watu mahiri kutoka Mkoa wa Kilimanjaro (UVIKI)umetoa msaada wa vitu mbalimbali pamoja na kuwalipia bima za Afya Kwa mwaka mzima watoto kumi wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi katika taasisi ya tiba ya mifupa ,Muhimbili (MOI),jijini Dar es salaam. 


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada huo, Makamo mwenyekiti wa umoja huo, Severini Mushi amesema wameamua kutoa msaada huo Kwa Watoto hao kama zawadi baada ya kuona Wana uhitaji.


Amesema kuwa wao kama umoja watu mahiri  kutoka Mkoa wa Kilimanjaro(UVIKI) waliona ni vyema kutumia siku ya leo ambapo umoja huo unafanya mkutano wake mkuu wa mwaka, uende sambamba na kuwasaidia watoto wenye vichwa vikubwa na migogo wazi kupata bima za Afya Kwa mwaka mzima pamoja na vitu mbalimbali ikiwemo, mchele, sabuni, Maziwa, Nguo, Sukari pamoja na vitu vingine walivyovitoa. 


"leo tunafanya mkutano wetu mkuu wa kufunga mwaka Kwa hiyo kabla hatujaenda jioni kwenye hafla ya mkutano huo,tukasema tushiriki na wenzetu wa hapa MOI Kwa ajili ya watoto wenye mgongo wazi na vichwa vikubwa, Kwa hiyo tuliomba nafasi na tunashukuru wakatupa na tumeleta zawadi vifaa mbalimbali hitajika na tumelipia bima Kwa watoto kumi na tumefika na tumekuta baadhi  watoto wengine hawana bima kutokana na changamoto ya vyeti hivyo tunaiomba wizara wanaweza kutusaidia kutoa kibali maalum kama mtu anawiwa tuwakatie bima hata wale wengine waliolazwa hapa,ambao wametoka mikoani na hawana vyeti vya kuzaliwa"alisema Bw Mushi 


Kwa upande wake Katibu mkuu wa (UVIKI),Godfrey Saleko amesema waliguswa na kuwiwa kutoa msaada huo na kuwalipia bima za Afya Kwa watoto hao baada ya kuona taarifa  katika vyombo vya habari kuwa Kuna watoto wana mahitaji mbalimbali wanaotokana na tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi, hivyo baada ya kuona taarifa hizo wakaamua kuwatembelea watoto hao, kuwapatia msaada wa vitu mbalimbali pamoja na bima za Afya. 


"sisi kama (UVIKI),pia tumekuwa na utaratibu huu na Kwa mwaka huu tumeona tufanye hivyo ili kuhamasisha jamii na wengine ambao wana nafasi kama sisi waweze kuja kuwaona na kuwasaidia hawa watoto Kwa sababu hawa watoto wakati mwingine waathiriwa na MALEZI ya upande Mmoja wa mama baada ya baba zao kuwakimbia na kutekeleza familia baada ya kuona matatizo hayo ya watoto"alisema Bw  Saleko.


Amesema kama jamii italichukulia suala la watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi Kwa umakini mkubwa tatizo hilo litamalizika Kwa kiasi Fulani katika jamii huku akitoa wito Kwa watu, wadau mbalimbali zikiwemo taasisi zenye mapenzi mema kuwa na utaratibu wa kuwatembelea watoto hao ili wapate nafasi muhimu ya kuwasaidia.


Naye Afisa ustawi wa jamii mwandamizi wa taasisi ya tiba ya mifupa,Muhimbili, (MOI) ameushukuru umoja huo Kwa misaada waliyoitoa ikiwemo bima za Afya na kuongeza kuwa umeonyesha ni jinsi gani watu wa mkoa wa Kilimanjaro walivyo na mioyo ya kuwasaidia wasiojiweza na wagonjwa.


"Kwa leo tumefurahi sana kuwapokea wageni, hasa hawa wanaume imekuwa kawaida kwamba wanakuja wamama makundi mengi yanayokuja hapa, lakini leo tumefurahi kuona wamekuja akina baba, wakina baba huwa wanaogopa kuwalea wagonjwa lakini hawa wameonyesha mfano mzuri na zawadi zao tumezipokea Kwa niaba ya watoto na Kwa niaba ya taasisi tunasema asanste."aliongeza Afisa huyo ustawi wa jamii (MOI)


Aidha ameitaka jamii kutembelea taaisi ya Moi ili kupata elimu ya namna ya kuzuia tatizo la vichwa vikubwa na migongo wazi kwani linazuilika huku akiiasa jamii hususan wanawake wanaotegemea kupata ujauzito  kutumia vidonge vya  folic acid miezi mitatu kabla ya kupata ujauzito ili kuzuia kuzaliwa Kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.


Akizungumza Kwa niaba ya wazazi ambao watoto wao Wana matatizo ya vichwa vikubwa na migongo wazi, Moja ya wazazi hao ambaye amejitambulisha Kwa jina la Sauda Rashidi ameushukuru umoja huo wa watu mahiri kutoka Kilimanjaro (UVIKI) Kwa kuwakumbuka watoto wao Kwa kuwapatia misaaada ya vitu mbalimbali pamoja kuwakatia bima za Afya Kwa mwaka mzima, akiongeza kuwa wao kama wazazi wameupokea Kwa mikono miwili msaada huo ambao Kwa kiasi kikubwa utawasaidia watoto wao ambao wamelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika taasisi ya tiba ya  mifupa (Moi).


"kiukweli nawashukuru sana Kwa misaada  waliyotupatia na Mungu atawabariki Kwa kutoa sehemu ya fedha zao kuwasaidia watoto wetu, akiwemo mtoto wangu ambaye ana tatizo la kichwa kikubwa" aliongeza Mzazi huyo.

Post a Comment

0 Comments