Na: Sheila Ahmadi
Naibu Waziri wa Uchukuzi David kihenzile amemtaka Mkandarasi Xiamen Ongoing Construction Group Co. Kutoka China anaejenga Bandari ya Mbamba bay kumaliza ujenzi wa bandari hiyo kwa wakati kama inayoonyesha kwenye Mkataba.
Kihanzile ameyasema hayo mara baada ya kutembelea eneo la Ujenzi wa Bandari ya Mbamba bay ambayo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Januari 2027 na kugharimu shilingi Bilioni 80.8.
"Nimeridhishwa na maandalizi ya Ujenzi wa Bandari hii hivyo mnatakiwa kumaliza ujenzi wa bandari kwa wakati kama inavoelekezwa kwenye Mkataba ili wananchi waweze kutumia bandari hii kibiashara na kunyanyua maendeleo ya Mbamba bay.’’ Alisema Kihenzile.
Aidha Kihenzile amemtaka mkandarasi huyo Xiamen Ongoing Construction Group Co. Ltd aweze kuhakikisha anatoa ajira kwa vijana wa eneo hilo ili kuweza kupata ushirikiano mzuri katika utekelezaji wa Mradi huo .
Naye Mbunge wa Nyasa Stella Manyanya ameishukuru serikali kwa Ujenzi wa Bandari hiyo kwani utaweza kusaidia shughuli za kibiashara katika kukuza ma eneo yaliyopo karibu ,pia ameomba kuboresha Miundombinu ya barabara katika eneo lote linalozunguka Bandari ya Mbamba bay.
Ametoa taarifa hiyo ya Mradi Meneja wa Bandari ya Ziwa Nyasa Manga Gassaya amesema kuwa katika utekelezaji wa Mradi huo wametenga fedha kiasi cha shilingi milioni miambili kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Msingi karibu na eneo la mradi ambao unatekelezwa
“Katika kushirikiana na jamii tumetenga shilingi milioni miambaili kujenga shule iliyopo karibu Bandari ili iendane na Ujenzi wa bandari ya inayojengwa Alisema Ngassaya.
Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay ukimakilika inategemewa kuwa Kati ya Bandari kubwa katika ziwa Nyasa na kuwa makao makuu ya Bandari zote katika ziwa Nyasa kwa Upande wa Tanzania.



0 Comments