Kyombiya: CCM Tabata Kimanga Kupitishwa kwa Bajeti ni Kichocheo katika Mafanikio

 


Na Francisco Peter

Diwani wa Tabata Kimanga, Pastory Kyombiya, ambaye anatoka katika Halmashauri ya ilala kupitia Chama cha Mapinduzi  (CCM) amesema kuwa bajeti iliyopitishwa ikiwa na makadirio mazuri kwa mwaka 2014/2025  itaenda kutekeleza miradi mingi  .

Akizingumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam  mwanzoni mwa wiki hii  alisema  bajeti hiyo italeta mageuzi makubwa ya kiuchumi katika kata yake huku ikochochea  kukamolika kwa umuhimu wa miradi ya miundombinu kama ujenzi wa barabara za lami na huduma za jamii.

"kufuatia kusomwa kwa makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024, ambayo yalipitishwa kwa matumizi mbalimbali ya halmashauri yetu sisi madiwani  tunaimani katika mipango ya maendeleo iliyowekwa," alisema Kyombiya.

Kwa upande wake, diwani wa Kata ya Gongolamboto, Lukas Rutahinirwa, ameelezea matumaini yake katika kuona miradi ya maendeleo ikitekelezwa kwa ufanisi, ikiwemo ujenzi wa soko kubwa na huduma za afya za kisasa.

Kwa jumla, madiwani hao wanaamini kuwa makusanyo mazuri ya fedha yatakwenda kutatua kero za wananchi kwa mwaka wa fedha 2024/25, na hivyo kuimarisha maendeleo katika manispaa hiyo.




Post a Comment

0 Comments