Na Sheila Ahmadi
Wakala wa mabasi. Yaendayo haraka Dart wamehitimisha Mafunzo rasmi ya teknolojia ya Tehama. kwa Waatalaamu na wengine. wachache. Lengo la mafunzo hayo ni kuweza kujikita kwenye. kadi Janja Ambazo zinaenda kutumia kwa njia ya nauli kwa abiria ambao wanatumia mabasi hayo yaendayo haraka .
Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu wa wakala wa mabasi yaendayo haraka Dart Dkt Athumani Kihamia alipozungumza na wana habari mara baada ya kufunga mafuzo hayo ambapo amesema kuwa kadi hizo za janja zitakuwa zinatumika kuingia getini ili kuweza kulinda teknolojia ya tehama kwani kuna baadhi ya watu wana tabia ya kudukua kwenye mifumo hiyo.
Dkt Kihamia amesema kuwa lengo letu kwa sasa tunaimarisha mifumo yetu ambayo ilikuwepo huko nyuma katika kuongeza waatalamu wa teknolojia kwani watalaamu hao wamepata mafunzo. Mahiri kutoka kwenye kampuni ya Advanide kutoka nchini India ambao wamekuja kutuwezesha katika Mafunzo na kubadilishana mawazo ya kitaaluma.
"Nichukue Fursa hii kuwaomba Wantazania na wanadar Es salaam waamini kuwa siku chache zijazo baada ya Mwezi wa sita tunaenda kuanza kutumia mageti yetu kwani tumeleta mageti kutoka nje ya nchi yaitwayo mageti janja zaidi ya 300. Ambapo mageti hayo yataenda kutumika katika nauli ili kuweza kuepusha kufuja kwa mapato na kuweza mazingira mazuri." Amesema Dkt Kihamia.
Nitoe wito kwa Madereva boda boda ambao wana tumia barabara za mabasi yaendayo haraka kuacha mara moja kwani kipindi cha miezi ya nyuma kulikuwa na ajali nyingi zinazosababishwa na madereva hao na wengineo wakiwemo katika kutumia barabara hizo Madereva daladala, wafanayakazi wa serikali hivyo acheni kutumia kipindi cha asubuhi na jioni kwani mnasababisha ajali na foleni huku zikiwa na mabasi maalumu ya kutumia njia hizo.
Naye Mkurugenzi wa Teknolojia, Habari. Na mawasialiano. kutoka Wakala wa mabasi yaendayo haraka Ng'wanashigi Gagaga ameongeza kuwa Mafunzo hayo yameweza kuchukua siku tano ikiwa na lengo ni kujenga uwezo Kupitia kwenye mfumo wa tehama ambao unatumia kadi janja hivyo ni mwendelezo wa Mafunzo kwani huko nyuma tulishawahi kufanya Mafunzo haya kwa Mwaka 2020 kwa vijana 200 Huku wengine wakifanya kazi Kwenye Taasisi mbalimbali.
Aidha ikumbukwe kuwa Mifumo hii inayoenda kutumiwa na abiria limetengenezwa na vijana ambao wameweza kupata Mafunzo.hayo huku mageti hayo yanaenda kusimikwa katika vituo kikiwemo kituo cha kimara korogwe kimesimikwa mageti kwa ajili ya kufahamu kuwa kadi ina fedha kiasi Fulani au hakuna kiwango cha pesa chochote kile " Amesema Mkurugenzi Gagaga
Kwa upande wake Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka kwenye Kampuni ya AdvanIde Wa Kadi janja Ducan chege amesema kuwa Huduma hii ya kadi janja tunatoa sehemu mbalimbali. duniani zikiwemo India,Tanzania na nyinginezo lakini kwa upande wa nchi ya TAnzania wamekuwa vinara katika huduma hii ya kadi janja hivyo nawapongeza kwa kuweza kutumia kadi janja kwa ajili ya Taasisi yao na abiria Kwa ujumla.
Kwa upande wake Mhitimu wa Mafunzo hayo Jackson Kazaura amesema kuwa tumefanya Mafunzo haya ya kadi janja Ambayo yatasaidia kwa upande wa wakala wa mabasi hayo katika kuboresha huduma Za nauli na ulinzi katika vituo vya mabasi yaendayo haraka hivyo Mafunzo hayo yametujenga kwa kiasi kikubwa




0 Comments