Dar es Salaam – Kampuni ya SMH Rail, inayoshirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC), imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watu wenye uhitaji kama sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Eid.
Msaada huo ulikabidhiwa leo tarehe 30, Machi 2025 jijini Dar es Salaam na Afisa Mawasiliano wa SMH Rail, Mariam Mwambo, ambaye alisema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kujali jamii na kusaidia wale wanaohitaji zaidi katika msimu huu wa sikukuu.
“Tunatambua umuhimu wa kusherehekea sikukuu kwa pamoja na jamii. Huu ni mchango wetu mdogo kwa wale wenye uhitaji, ili nao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid kwa amani na furaha,” alisema Mariam Mwambo wakati wa hafla ya makabidhiano.
Watu waliopokea msaada huo walionyesha furaha na shukrani kwa kampuni ya SMH Rail kwa moyo wa upendo waliouonyesha katika kipindi hiki muhimu cha kidini.
SMH Rail imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na TRC katika maendeleo ya sekta ya reli nchini, huku pia ikihimiza ushirikiano na jamii kwa kusaidia makundi yenye uhitaji kupitia misaada ya kijamii.




0 Comments