NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa kwa mwaka 2025 ndugu Ismail Ussi ameridhishwa na miradi mbali mbali ambayo imetekelezwa na Halmashauri ya Kibaha mji katika nyanja mbali mbali ikiwemo miundombinu ya barabara, afya, elimu pamoja na kutumia mapato ya ndani ya asilimia 10 katika kuvisaidia vikundi mbali mbali vya wajasiriamali kwa lengo la kuweza kuwainua kiuchumi.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kitaifa ameyabainisha hayo baada ya mbio za mwenge wa uhuru kuweza kupita katika miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwa pamoja na kuweza kupata fursa ya kuikagua,kuitembelea, kuizindua na mingine kuiwekea mawe ya msingi ambayo imegusa katika nyanja ya elimu, miundombinu ya barabara pamoja na huduma nyingine za kijamii.
'Kwa kweli mimi pamoja na wakimbiza mwenge wa uhuru kitaifa tumeweza kujiridhisha na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo tumeweza kujionea na kwa kweli wameweza kujitahidi kwa kiasi kiubwa katika suala zima la kutumia fedha ambazo zimetolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo, ya afya, elimu, miundombinu ya barabara pamoja na kuwasaidia vikundi vya vijana,"amesema kiongozi huyo wa mbio za Mwenge.
Amebainisha amewahimiza viongozi na watendaji wote kuhakikisha kwamba wanatumia vizuri fedha ambazo zinatengwa na serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kwambawaendelee kuvisaidia vikundi vya wajasiriamali kupitia fedha za mapato ya ndani kuwawezesha fursa za mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassana kwa kuweza kutenga fedha nyingi ambazo zimekwenda kuleta mabadiliko chanyaa ya kimaendeleo katika kuwasaidia wananchi changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka amesema kwamba kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan miradi mbali mbali ya maendeleo imeweza kutekelezeka kwa kiwango kikubwa ikiwemo huduma ya maji safi na salama,nishati ya umeme, miundombinu ya barabara pamoja na huduma za kijamii.
Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa zimeweza kupita katika Halmashari ya Kibaha mji na kutembelea miradi ya maendeleo ikiwemo umeweka jiwe la msingi katika zahanati ya Kilimahewa kata ya Tangini, uzinduzi wa kisima cha maji Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani tumbi,kutembelea mradi wa ujenzi wa kiwango cha lami kata ya sofu, mradi wa vijana kata ya Tangini sambamba na mradi wa maegesho ya magari eneo la misugusugu.




0 Comments