MOYO WA MSAMAHA NDIO UTAKAOLIJENGA TAIFA LETU - DKT. NCHIMBI




Katika tafakari ya kipekee ya Sikukuu ya Pasaka, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, alitoa wito mzito unaogusa misingi ya utu, imani na ujenzi wa taifa. 


Alitoa rai kwa Watanzania, hususan Wakristo, kutambua nguvu ya msamaha kama msingi wa kulijenga taifa imara.


“Yesu hana hatia na hana dhambi, lakini anasema ‘natoa maisha yangu, maisha ya sadaka safi kwa ajili ya maisha ya watu wengine wenye dhambi’,” amesema Dkt. Nchimbi, akisisitiza kuwa sadaka ya Kristo ni somo la upendo na msamaha wa kweli.


Alieleza kuwa sala ya Baba Yetu, inayotamkwa na kila Mkristo, hubeba agizo la kusameheana. 


Hata hivyo, alitahadharisha juu ya unafiki wa kuomba msamaha kwa midomo huku mioyo ikiwa imejaa chuki. 


“Unamaliza tu sala ya Baba Yetu, hapohapo unaanza kukumbuka mwenzako aliyekukosea mwaka juzi,”aliseema.


Kwa msingi huo, Alitoa  ujumbe wa kipekee unaosema:


“Msamaha unaotoka kwa Bwana Yesu unaimarishwa na msamaha unaotoka kwako kwa ndugu zako, kwa jirani zako, kwa rafiki zako na kwa adui zako. Moyo wa msamaha ndio utakaolijenga taifa letu.”


Katika siku hii takatifu ya Pasaka, Dkt. Nchimbi amewahimiza wananchi kusema kwa dhati: “Mchango wangu kwa taifa langu ni kusamehe walionikosea, kwa sababu najua hiyo ndiyo sadaka kubwa kuliko zote kwa Baba Mungu wa mbinguni"

Post a Comment

0 Comments