Dar es Salaam
Kampuni ya mapambo ya ndani, Young Millionaire Interior, imezindua rasmi duka lake jipya tarehe 10 Januari, 2025, katika eneo la Sinza Mori, jijini Dar es Salaam, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa bidhaa na huduma zake kwa wateja wa majumbani na kibiashara.
Uzinduzi huo ulifanyika katika hafla ya hadhi ya juu iliyohudhuriwa na watu mashuhuri, wafanyabiashara wakubwa pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya mapambo ya ndani, hali iliyoonesha kuongezeka kwa imani ya soko kwa chapa hiyo na mchango wake katika kukuza tasnia hiyo nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, uongozi wa Young Millionaire Interior ulieleza kuwa kufunguliwa kwa duka hilo jipya ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kupanua biashara, kuimarisha uwepo wake katika maeneo muhimu ya kibiashara na kuwahudumia wateja kwa ufanisi zaidi. Aidha, kampuni ilitangaza ofa maalum ya punguzo la asilimia 50 kwa bidhaa mbalimbali za mapambo kama njia ya kusherehekea uzinduzi huo.
Ofa hiyo imepokelewa kwa mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi, ambapo wateja wengi walijitokeza kunufaika na fursa hiyo, jambo linaloonesha uhitaji mkubwa wa bidhaa za mapambo ya kisasa na zenye ubora wa hali ya juu.
Kwa mujibu wa wadau wa sekta hiyo, hatua ya Young Millionaire Interior kuendelea kupanua shughuli zake ina mchango chanya katika kukuza uchumi, kuongeza ushindani wa kibiashara na kuimarisha ubunifu katika sekta ya mapambo ya ndani nchini Tanzania.








0 Comments