ASASI YA KIRAIA ZAONYWA MISAADA YENYE VIASHIRIA VYA KUUNGA MKONO USHOGA NA UGAIDI

 



Serikali imeyataka mashirika yasiyo ya kiserikali nchini kuachana na misaada kutoka kwa wafadhili yenye viashiria vya uvunjifu wa tamaduni za Kitanzania ikiwemo mapenzi  ya jinsia moja na Ushoga.






Kwa kipindi cha hivi karibuni uvunjifu wa utamaduni wa Kiafrika umeonekana kutamalaki hali iliyowaibua wadau ikiwemo serikali kutoa mafunzo kwa mashirika hayo kuhusiana na madhara yatokanayo na ukiukwaji wa tamaduni nchini.


Wakili wa serikali kutoka ofisi ya msajili mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Denis Bashaka amesema serikali haitowafumbia macho mashirika yanayoenda kinyume na sheria na kanuni za uendeshaji mashirika hayo.




Kwa upande wake Mratibu taifa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini THRDC Onesmo Ole Ngurumwa amesema mafunzo hayo ni miongoni mwa mikakati ya kupambana na matendo yasiyofaa ikiwemo utakatishaji fedha na kujenga uelewa kw asasi hizo juu ya vyanzo vya fedha wanazopokea.



Jumla ya mashirika yasiyo ya kiserikali 40 yanapatiwa mafunzo ya siku mbili jijini Dar es Salaam kutoingia katika mtego wa utakatishaji fedha pamoja na kutumika kufadhili ugaidi ambapo lengo kufikia mashirika yote nchi nzima.

Post a Comment

0 Comments