Mwanza mwenyeji Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Kitaifa

 Mwanza mwenyeji Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Kitaifa 


Uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani Kitaifa kufanyika Machi 14 Mkoani Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe.Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania





Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amewataka watumiaji wote wa barabara katika Mkoa wa Mwanza kuzingatia vyombo vyao vya moto vinakaguliwa mara kwa mara ili kuepusha ajali zinazotokana na ubovu wa vyombo hivyo.


Malima amewaomba wananchi wa mikoa ya kanda ya Ziwa kuhudhuria Maadhimisho ya Wiki na nenda kwa Usalama kufika viwanja vya Furahisha ili waweze kupata elimu ya Sheria, Kanuni na taratibu za Usalama Barabarani 




Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yana kauli mbiu isemayo, Tanzania bila ajali inawezekana - Timiza wajibu wako


Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Ramadhani  ng'anzi amewataka wamiliki wa vyombo vya moto kufika maeneo yaliyotengwa kwa ajli ya ukaguzi wa vyombo hivyo lengo likiwa ni kuondoa ajali ambazo zinaepukika

Post a Comment

0 Comments