MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, viwango vya usahihi wa utabiri wa hali ya hewa kwa ujumla vimeongezeka na kufikia asilimia 88.5, ambapo katika msimu wa mvua za vuli 2022, viwango vya usahihi vilikuwa asilimia 94.1.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotelewa kwa vyombo vya habari na mamlaka hiyo imesema viwango hivi ni juu ya kiwango cha usahihi wa utabiri kinachokubalika na shirika la hali ya hewa duniani (wmo) cha asilimia 70.
Imeelieza kuwa ongezeko hili la usahihi wa utabiri unazifanya huduma za hali ya hewa zinazotolewa nchini kuwa za uhakika na kuleta mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta zote za kiuchumi na kijamii nchini zinazotegemea hali ya hewa.
Pia taarifa hiyo imesema kuongezeka kwa usahihi wa utabiri kumetokana na jitihada za serikali kuwekeza katika kusomesha wataalam wa hali ya hewa, ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kuandaa utabiri pamoja na kuongezeka kwa mtandao wa vituo vya kupima hali ya hewa.
Aidha, mamlaka imeendelea kutoa utabiri wa msimu na tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa usahihi na ubora hivyo kuchangia kupunguza athari kwa watu na mali zao.
Pia mamlaka hiyo imefanikiwa kuboresha mazingira ya kazi kwa kukarabati vituo saba vya hali ya hewa vilivyopo katika mikoa ya Singida, Songwe, Mpanda, Shinyanga, Songea, Mahenge na Tabora pamoja na nyumba tatu za wafanyakazi.
Vile vile imesema inaeendelea na uboreshaji wa miundombinu ya vifaa vya hali ya hewa kuendana na teknolojia na matakwa ya kimataifa ikiwemo kuondoa vifaa vyote vinavyotumia zebaki kwa kunua vifa 15 vya kidigitali vya kupimia mgandamizo wa hewa na vifaa 25 vya kidigitali vya kupima joto hewa.
Kuhusu uboreshaji wa miundombinu, mamlaka hiyo ilinunua rada nne za hali ya hewa ambapo ufungaji wa rada mbili katika mikoa ya kigoma na mbeya unaendelea huku utengeneza wa rada mbili kiwandani nchini marekani ukifikia asilimia 63
Kumamilika kwa rada hizo nne za hali ya hewa kutakamilisha lengo la muda mrefu la TMA kuwa na rada saba za hali ya hewa kwa nchi nzima.
.jpeg)
0 Comments