LENGO LA VIJANA INNOVATIONS NI KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI– Dorcas Mshiu

 


VIJANA INNOVATIONS imeendesha mafunzo maalumu kwa vijana yaliyolenga kuongeza thamani ya vijana na kuwajengea uwezo wa kuwa tayari kiuchumi, yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam


Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Dorcas Mshiu alisema mpango huo umeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata maarifa ya ujasiriamali, ubunifu na mbinu za kujitegemea 


Alieleza kuwa kupitia mafunzo hayo, vijana wanapata elimu inayowasaidia kutumia fursa zilizopo katika jamii, kuanzisha biashara pamoja na kujijengea misingi imara ya maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.


Mshiu alisisitiza kuwa vijana wanapaswa kuwa tayari kiuchumi kwa kutumia ujuzi na maarifa wanayopata, akiwahimiza washiriki kuyatumia mafunzo hayo kama chachu ya mafanikio yao ya baadaye.



Mafunzo hayo yamewakutanisha vijana mbalimbali waliopata nafasi ya kujifunza, kushirikiana uzoefu na kujenga mtandao wa fursa za maendeleo.

Post a Comment

0 Comments