UWT BAGAMOYO KUCHELE YAPANIA KUFANYA KAMPENI ZENYE TIJA KATIKA UCHAGUZI MKUU 2025





NA VICTOR MASANGU,BAGAMOYO 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Wilaya  ya Bagamoyo Mariam Mkalì  amewaasa wanawake Ä·uhakikisha kwamba kuweka misingi mizuri ya kwenda kufanya kampeni za kistaarabu kwa kuzingatia kanuni na taratibu hasa  katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Kauli  hiyo ameitoa wakati wa kikao cha Baraza la kawaida la jumuiya ambalo limefanyika katika  Kata ya Msata na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na jumuiya zake.

Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba kwa sasa wanapaswa kuwa kitu kimoja  na kushikamana kwa hali ya upendo na amani   katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu.

" Kikubwa ninachowaomba wanawake wenzangu  tushikamane hasa katika  kipindi chote  cha uchaguzi na kwamba uchaguzi  usiwe sababu za kutoleana lugha chafu,"amebainisha Mwenyekiti.

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya hiyo ya UWT Wilaya ya Bagamoyo  Catherine Makungwa amewahimiza wanawake kunitokeza kwa wingi katika kumpa  kura nyingi za kishindo Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Nawashukuru kwa dhati  Wabunge, Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa Mariam Ulega na Madiwani wote  kwa michango yao mikubwa ambayo yameitoa  katika kusaidia Jumuiya hiyo kufanikisha shughuli zao  mbali mbali,"

"Pia namshukuru Mbunge wetu Muharami Mkenge, Ridhiwani, Hawa Mchafu, Dkt. Harris na Subira Mgalu ambao wamekuwa msaada mkubwa katika Jumuia yetu, wakiwemo wadau mbalimbali," amesema Makungwa.

Kwa upande wao Madiwani wastaafu  wa Viti Maalumu ambao wamemaliza  muda wao wamesoma taarifa zao za Utekelezaji katika kipindi cha miaka mitano cha kuanzia mwaka 2020 hadi 2025.


               

Post a Comment

0 Comments