NEC YAWANOA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI BAGAMOYO,,DAR ES SALAAM,MKURANGA,RUFIJI,CHALINZE

 



Na Magrethy Katengu--

Dar es salaam

TUME huru ya Taifa ya uchaguzi NEC imewataka waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi ngazi ya Jimbo , na maofisa ununuzi kutenga sehemu ya muda wao kwa kusoma katiba ,Sheria na maelezo mbalimbali yanayotolewa na Tume hiyo.

Agizo hilo limetolewa Dar es salaam Julai 21,2025 na  Mjumbe wa Tume huru ya Uchaguzi  Balozi Omar Ramadhan Mapuri  wakati wa ufungnzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi  wapatao 108 kutoka halmashauri za Bagamoyo ,mkuranga, Rufiji, Chalinze za mkoa wa Dar es salaam na Pwani.

" Mafunzo haya yakakwenda ni kwa lengo la kusoma katiba , Sheria na maelezo mbalimbali yanayotolewa na Tume Ili mnapotoka hapa muweze kuogoza na kusimamia vyema uchaguzi utakao kuwa huru na haki" Amesema Balozi Omar

Hata hivyo Tume  huru ya Taifa ya uchaguzi imetenga siku hizi tatu kuwapatia mafunzo haya kama sehemu ya kuwaongezea  maarifa na uzoefu kwenye kipindi chote cha uchaguzi mkuu kwa kuzingatia Sheria na kanuni za uchaguzi .

Sanjari na hayo   Sheria  na miongozo kwa wasimamizi wa uchaguzi inawataka wapiga kura kutoka kwenye maeneo ya kata na mikoa kushiriki zoezi la upigaji kura linapaswa kuwa la haki kwa raia wa Tanzania.

Aidha ameipongeza Tume huru ya uchaguzi na jukumu la kusimamia pamoja na kuratibu uendeshaji wa chaguzi kwa mujibu wa Sheria kulinda Democrasia kwa manufaa ya wananchi , vyama vya siasa vyote na wagombea

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume hiyo, Giveness Aswile, amesema mafunzo hayo yalipangwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza yalifanyika Julai 15 hadi 17, na awamu ya pili ya kuanzia Julai 21 hadi 23 mwaka huu.





Post a Comment

0 Comments