MWENYEKITI CCM BAGAMOYO AKEMEA VITENDO VYA VIONGOZI KUCHAFUANA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII




NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

Mwenyekiti wa  chama cha mapinduzi  (CCM) Wilaya Bagamoyo Ndugu Aboubakary Mlawa amewataka wana CCM kuachana na tabia ya kuwa na siasa za  fitina na kuchafuana kwenye mitandao ikiwemo kwamba kitahakikisha kwamba  hakitoteua wagombea kwa mihemko ya mitaani hama  kupitia mitandao ya simu.

Mlawa ameyasema hayo  wakati wa kikao cha  mkutano wa Halmashauri kuu ya  Kata ya  Mapinga  juu kuhusiana na  utekelezaji wa ilani kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa 2020 hadi 2025 na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama, viongozi wa serikali, pamoja na viongozi wa dini.

Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba kwa sasa chama kimejipanga kwa ajili ya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2025 na kuwahimiza wanachama wa ccm kuhakikisha wanawachagaua wagombea  wenye sifa ambao wataweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi.

"Kitu kikubwa ninawaomba wanachama na viongozi kuachana na vitendo vya kufanyiana siasa za kuchafuana na fitina na kuhakikisha wanaachana kabisa na siasa za kwenye mitandao na lengo letu kubwa ni khakikisha kwamba katika uchaguzi mkuu kuna kuwa na hali ya amani na utulivu,"amebainisha Mwenyekiti Mlawa.

Aidha Mlawa amesema kwamba  kumekuwepo  na  tabia kwa baadhi ya wana ccm kutumia  makundi ya mitandao ya kijamii kwa kuanza kulazimisha wagombea wao ndio waweze kuteuliwa  katika nafasi mbali mbali kitu ambacho amekemea vikali kwani wanapaswa kuzingatia taratibu na kanuni za chama.

"Kitu kikubwa ninachowaomba wana  ccm kuhakikisha kwamba msiwateuwe kabisa  watu kwa  kupitia njia za  magroup ya mitandao ya kijamii kwani pamoja na kuachana kabisa na kuwa na siasa za kuchafuana na badala yake ni kuweka mikakati madhubuti ya kumpa kura nyingi Rais wetu wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan aweze kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020,"amesema Mlawa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mapinga Dismas Dismas  amesema kwamba katika kipindi  miaka mitano ameweza kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta mbali mbali ambayo imeweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi kuweza kupata huduma za maji,afya, elimu pamoja na miundombinu ya barabara.

                       

Post a Comment

0 Comments