MBETO HAMIS MBETO AWASILI MASHINDANO YA 3 YA KUHIFADHI QURAN DAR ES SALAAM

 











Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Mbeto Hamis Mbeto, amewasili katika mashindano ya tatu ya kuhifadhi Quran yaliyoandaliwa na Imaadud-Diin Foundation yanayofanyika leo Februari 28, 2026 jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yamewaleta pamoja washiriki kutoka sehemu mbalimbali wakishindana katika kuhifadhi na kusoma Quran Tukufu, yakilenga kuhamasisha jamii hususan vijana kuzingatia maadili ya dini na kukuza elimu ya Kiislamu.

Uwepo wa Mbeto umeongeza uzito wa tukio hilo, huku waandaaji wakisisitiza kuwa ushiriki wa viongozi wa kisiasa na kijamii huchochea vijana kushiriki shughuli za kidini na kuimarisha mshikamano wa jamii.

Kwa mujibu wa Imaadud-Diin Foundation, mashindano hayo ni sehemu ya juhudi za kukuza malezi ya kiroho, kuendeleza utamaduni wa kuhifadhi Quran na kujenga jamii yenye maadili mema.

Post a Comment

0 Comments