Na Sheila Ahmadi
Shirika la Reli Tanzania TRC imezindua rasmi kampeni ya kuanza kutoa huduma ya usafiri wa treni za kisasa (SGR) kutoka Dar es salaam hadi mkoani morogoro mwezi juni tarehe 14 ambapo shirika hilo limesema kuwa ujio wa treni hizo za kisasa hazitoweza kuzuia vyombo vingine vya usafiri ikiwemo Mabasi yaendayo mikoani na Treni ambazo zilikuwa zinatumika kipindi cha nyuma kwani treni hizo zinasaidia katika kusafirisha abiria kutoka Dar es salaam kwenda mikoa jirani ikiwemo morogoro, na kigoma.
Akizungumza. Jijini Dar es salaam Mkurugenzi. Mtendaji wa shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema kuwa leo tunazindua rasmi kampeni hii ya kuanza kutoa huduma za treni ya kisasa kutoka Jijini Dar es salaam kwenda. Mkoani morogoro juni 14 safari zetu zinaenda kuanza rasmi hivyo watanzania tunatakiwa kupanda treni zetu kwa bei ya shilingi elfu 13000 hivyo tunawakaribisha katika kupanda treni zetu na kupatiwa huduma bora pindi tuwapo kwenye usafiri huo wa Treni.
Kampeni hii ya uzinduzi Ina lengo ya kutoa huduma za SGR ikiwemo na ulinzi kwenye treni hizo pia sisi kama shirika tunaomba wananchi tushirikiane katika kutunza. Miundombinu kwani treni hio ni Mali ya watanzania na imejengwa kupitia kodi za. Watanzania kwa kutumia huduma za TRC ili liwe pato la kitaifa pia tutaangalia ubora wa miundombinu na usalama wa abiria "Amesema Mkurugenzi kadogosa .
"Sisi kama Shirika tumejipanga kuanza safari. Za Dar es salaam kwenda Dodoma mwezi julai 25 Mwaka huu. 2024 huku tukiendelea kuchukua hatua kadhaa ikiwemo hii ya Tarehe 14 juni katika kuanza kutoa safari kupitia treni hiyo hivyo katika kutimiza Agizo La Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt samia suluhu hasani shirika linatoa pongezi kwa kuweza kutoa huduma ya Treni katika viwango vya kimataifa SGR. Kutoka Dar es salaam kwenda morogoro tarehe 14 juni mwaka huu. Huku uzinduzi huo ukiwa na Kaulimbiu isemayo kuwa TWENDE TUKAPANDE TRENI YETU , TUITUNZE, TUITHAMINI.
Aidha kuanza kwa safari hizi kutoka Mkoani Dar es salaam kwenda mkoani morogoro. Ni sehemu ya kuendelea kujifunza kupitia Teknolojia mpya nchini na kujiridhisha na mifumo mbalimbali kabula ya kuanza safari rasmi za kutoka Dar es saalam kwenda Dodoma ifikapo tarehe 25 mwezi julai na kuanza safari baada ya shirika kujiridhisha na Miundombinu, vitendea kazi kwa maana ya vichwa vya mabehewa .
Vilevile Kadogosa Ametoa pongezi kwa Rais Dkt Samia suluhu na serikali kwa ujumla kwa kutumia utashi wake wa kisiasa kwani alitoa a had I kwa watanzania kuwa atamalizia vipande vya ujenzi ambavyo Amelita na kuanzisha vipande vingine hivyo serikali yetu imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo ya kisasa ikiwemo ujenzi wa makotupora .
Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka benk ya Tanzania commercial benk (TCB) Adam mihayo. amesema kuwa tuna furaha kubwa katika kushirikiana na shirika hili kwani ni muda mrefu sasa tunashirikiana katika mambo mbalimbali katika.kukuza uchumi wa nchi yetu kutoka kwenye shirika hili hivyo mimi kama Mkurugenzi wa benki ya TCB tumeaminiwa katika utendaji kazi kupitia kwenye utendaji wetu.
"Tumeingia kwenye makubaliano katika kuweza kutoa huduma kwa watumiaji wa Reli hiyo pia tukio hili limekuwa la kihstoria kwenye nchi yetu katika.kutimiza maono ya muda mrefu ya Rais Dkt samia kwa kutuletea Treni za SGR kwani reli yetu ni ya kwanza Afrika Mashariki ." Amesema Mkurugenzi mihayo.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Tehama kutoka TRC Lilian Msele ameongeza kuwa tuna end a kutoa huduma za tiketi kwa kontrol namba kwa abiria lengo ikiwa ni kuepukana na changamoto ndogondogo pia abiria ambao wanaenda kutumia treni hizo wasiwe na mizigo mikubwa zaidi ya kilo 30 na hatutoruhusu kubeba vyakula lakini watoto chini ya miaka 5 tunaruhusu kubeba maziwa na uji
.jpg)





0 Comments