ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 417.8 ZATUMIKA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA CHAANI

 


ZANZIBAR

Zaidi ya shilingi milioni 417.8 zimetumika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo katika Jimbo la Chaani, Wilaya ya Kaskazini A, ndani ya kipindi cha miezi nane kupitia ushirikiano kati ya Mbunge wa Jimbo hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed, pamoja na wahisani mbalimbali.

Fedha hizo ni sehemu ya juhudi za kutekeleza maono ya kuboresha ustawi wa wananchi na kuongeza kasi ya maendeleo katika jimbo hilo.

Akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na shughuli za maendeleo za jimbo katika kikao kilichofanyika Tawi la CCM Chaani Masingini, Wilaya ya Kaskazini A, Naibu Waziri Ayoub Mohammed amesema fedha hizo zimeelekezwa katika maeneo mbalimbali muhimu.

Ametaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na huduma za jamii, elimu, uwezeshaji wananchi kiuchumi, afya, kilimo, usafiri na usafirishaji, habari na mawasiliano, maji safi na salama, pamoja na shughuli za uhamasishaji wa chama.

Amesema utekelezaji huo unaendelea kuwa sehemu ya jitihada za kuhakikisha wananchi wa Jimbo la Chaani wanapata huduma bora na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.

Post a Comment

0 Comments