Wananchi wa Mkoa wa Morogoro na maeneo ya jirani wamealikwa kujitokeza kwa wingi kushiriki Kongamano la Kiroho la “Inua Uzao Wako”, litakalofanyika Wilaya ya Gairo kuanzia Julai 23 hadi 26 mwaka huu.
Akizungumza kuhusu kongamano hilo, Prophet Joseph Mtapi amesema lengo ni kuwakutanisha waumini na wananchi kwa ajili ya mafundisho ya Neno la Mungu, maombi na ibada za kumwabudu Mungu, ili washiriki wajengwe kiroho na kuimarisha imani yao.
Ameeleza kuwa kongamano hilo litakuwa na vipindi mbalimbali vya mafundisho, maombi na ushirika wa waumini, huku akiwakaribisha watu wote bila ubaguzi kushiriki katika tukio hilo.
Prophet Mtapi ametoa wito kwa wananchi wa Gairo, Morogoro na maeneo mengine nchini kujitokeza kwa wingi na pia kuwahamasisha ndugu, jamaa na marafiki zao kushiriki katika kongamano hilo.
Kwa mujibu wa waandaaji, maandalizi ya kongamano hilo yamekamilika, na washiriki wanatarajiwa kuwasili kutoka maeneo mbalimbali kwa ajili ya kushiriki katika siku hizo nne za ibada na mafundisho.
Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo, wananchi wanaweza kuwasiliana na Prophet Joseph Mtapi kupitia simu +255 753 071 863.
Karibu sana Gairo, Morogoro kuanzia Julai 23 hadi 26 kushiriki Kongamano la “Inua Uzao Wako”.


0 Comments