MBUNGE WA KAWE AKUTANA NA VIONGOZI WA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA KODI.

 


Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Geofrey Timoth amekutana na viongozi wa serikali ya wanafunzi chuo cha kodi kilichopo Mikocheni B Eneo la viwanda leo jalai 29, 2026.

Timoth amewapongeza viongozi hao kwa kuchaguliwa kuwa viongozi wa serikali ya wanafunzi chuo cha kodi, pia amewaambia asilimia kubwa ya viongozi wa Taifa hili wamewahi kuwa viongozi mavyuoni kama mlivyo nyinyi leo hii, amewataka waendelee kuwa viongozi hata pale ambapo wamemaliza mavyouni.


Aidha Timoth amewaasa wanafunzi hao kuwa na nidhamu mavyouni kwani nidhamu ni nguzo muhimu kaitka maisha ya mwanadamu, nidhamu huweka msingi imara ya mafanikio ya kitaaluma na malezi bora ya mwanafunzi pia amesema nidhamu ni muhimu sana kwa maendeleo kamili ya wanafunzi inachangia katika ufaulu wa kitaaluma , inajenga tabia njema na inamwaandaa mwanafunzi kuwa mtu mzima na mwenye tija katika jamii.

Timoth amewataka wanafunzi hao wawe wazalendo na Taifa lao wasijihusishe na vichochezi vyovyote ambavyo vinaashiria kuvuruga amani ya Taifa letu.

#kawempya

#kaweyetu

#ukwelinauhakika

#kazinaututunasongambele

Post a Comment

0 Comments