Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mama Asemewe Taifa, Henry John Manywili, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Semina ya Uzalendo, Maadili na Uongozi itakayowakutanisha wasomi wa vyuo na vyuo vikuu kutoka Wilaya ya Ubungo, Julai 4, 2026.
Semina hiyo itafanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana, ikiwa na lengo la kuwajengea vijana uzalendo, maadili mema na uwezo wa uongozi ili kuwaandaa kuwa viongozi bora wa taifa.
Kwa mujibu wa waandaaji, semina hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Mama Asemewe chini ya kaulimbiu isemayo "Wasomi Wazalendo, Taifa Imara," ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa lenye maadili, uwajibikaji na maendeleo endelevu.
Waandaaji wamewataka wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu wilayani Ubungo kujitokeza kwa wingi kushiriki semina hiyo ili kupata maarifa na uzoefu utakaowasaidia katika maisha yao binafsi, kitaaluma na katika kuandaliwa kuwa viongozi wa baadaye.


0 Comments