MJUMBE WA HALMASHAURI KUU CCM (W) YA UBUNGO ABEID ABEID AZUNGUMZA MIKAKATI NA VIJANA KUELEKEA USHINDI WA KISHINDO WA CCM.

 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ubungo kupitia kundi la vijana, Ndg. Abeid Abeid, azungumza na vijana katika kikao kazi kilichowakutanisha viongozi wa UVCCM wa matawi na kata, chini ya Mwenyekiti Shadrack Makangula, kwa lengo la kupanga mikakati ya kushawishi kura kutoka kwa vijana.


Katika kikao hicho, Abeid alimhimiza mgeni rasmi kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri na kuajiriwa endapo CCM itashinda kwa kishindo.














Mgeni rasmi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba, Mhe. @angellah_kairuki, aliwaeleza vijana vipaumbele vya Ilani ya CCM 2025-2030, ikiwemo:

Kuongeza ajira kwa vijana


Kuimarisha kongani za viwanda


Kukuza ubunifu na teknolojia


Kuanzisha SACCOS na kampuni za vijana


Kutoa mikopo ya 10% kupitia halmashauri


Kuanzisha vituo vya umahiri kwa vipaji vya michezo


Aidha, aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba kuhakikisha ushindi kwa wagombea wa CCM.






Post a Comment

0 Comments