UCHUMI WA BULUU: FURSA MPYA YA AJIRA, BIASHARA NA USTAWI WA WANANCHI

 






Kongamano hilo la Kitaifa la Wadau wa Uchumi wa Buluu lilifanyika tarehe 10 Septemba, 2025, likihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka pande zote za Muungano. 

Akizindua rasmi kongamano hilo, Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Abdallah Mitawi, alieleza msimamo wa serikali kuhusu maendeleo ya uchumi wa buluu.

"Serikali imedhamiria kutumia fursa kubwa zilizopo katika rasilimali za bahari na maji ya ndani kwa maendeleo endelevu ya Taifa," alisema Bw. Mitawi. "Uchumi wa buluu ni injini mpya ya maendeleo ya Tanzania. Ukitumiwa ipasavyo, unaweza kuongeza ajira, kukuza biashara na kuimarisha ustawi wa wananchi."


Kongamano hili liliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Uchukuzi kupitia Chuo cha Bahari cha DMI, na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Zanzibar. Lengo kuu lilikuwa kuwakutanisha wadau muhimu kutoka sekta mbalimbali kwa ajili ya kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja ya kuendeleza sekta ya uchumi wa buluu nchini.


Kupitia majadiliano ya kitaalamu, washiriki waliweka msisitizo juu ya matumizi endelevu ya rasilimali za baharini na maji ya ndani kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha Kaulimbiu ya kongamano hilo ilikuwa "Bahari Yetu, Fursa Yetu, Bahari Yetu", kauli ambayo imeongoza juhudi za maendeleo katika sekta ya uchumi wa buluu tangu mwaka 2021 hadi 2025.



Post a Comment

0 Comments