CCM PWANI YAMPONGEZA RAIS DKT. SAMIA KWA KUDUMISHA AMANI KWA TAIFA


Na Victor Masangu, Pwani

Katibu wa siasa,uenezi na Mafunzi wa chama cha mapinduzi (CCM) Dkt. David Mramba amewaasa wananchi hususan vijana kuwa wazalendo na nchi yao na kuachana kabisa na vitendo vya kutumika kwa maslahi ya makundi ya watu wengine na badala yake kuhakikisha wanaweka misingi ya kuwa walinzi na kudumisha amani.

Dkt. Mramba ameyabainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na masuala ya wananchi kuwa na jukumu la kulinda amani katika maeneo yao na kuwahimiza wanapaswa kuzingatia katiba na sheria na kutojiingiza katika vitendo ambayo vinaweza kkuhatarisha usalama wa maisha yao

"Suala la amani ni jambo la muhimu sana katika yetu hivyo niwasihi wananchi wote wa Mkoa wa Pwani msikubali hata kidogo kuwashawishi kufanya vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kuhatarisha usalma wa maisha , ikiwemo mali pamoja na uchumi wetu kwani amani ni msingi mkubwa wa maendeleo,"amebainisha Dkt. Mramba .

Aidha Katibu huyo amewahimzia wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda watoto wao na kwamba kila kijana anapaswa kufikiria mustakabali wake ikiwa pamoja na kuweza kulinda amani na kuitunza katika maeneo yao wanayoishi.

Pia Katibu huyo amebainisha kwamba Mkoa wa Pwani umebarikiwa kuwa na lango muhimu la uchumi wa Taifa wakiwemo wakulima,wafugaji ,wavuvi, na wafanyabiashara na wawekezaji kwa hiyo kunahitajika kuwa na mazingira mazuri yenye amani na utulivu.

Mramba pia amewaomba wananchi wote wa Mkoa wa Pwani kuendelea kuwa walinzi wa amani na kwamba wanatakiwa kushirikiana bega kwa bega na vyombo vya dola katika kulinda usalama na tuendelee kujenga Tanzania yenye umoja na mshikamano na maendeleo.

Aidha Katiba amebainisha kwamba chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kinampomgeza na kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa mstari wa mbela katika kudumisha hali ya amani na utulivu katika Taifa la Tanzania.

                                                  

                                                              

Post a Comment

0 Comments