Kwenye Taasisi za Benki
Na Mwandishi Wetu
Vichocheo vya kuwepo kwa amani nchini kimekuwa ni namna pekee ya utulivu wa wamachinga Kariakoo jijini Dar es Salaam kuizungumza vizuri serikali nchini kuwa ni kichocheo cha wao kufanya ujasiriamali wenye tija.
Akizungumzia Dar es Salaam juu ya michakato katika hatua mbali mbali za kuendelea kujipatia vipato wajasiriamali Katibu wa Chama Cha Wamachinga Kariakoo (KAWASSO) Augustino Choga amesema uwepo wa amani nchini imechagiza kuwa na mawasiliano mazuri kwani mshikamano wa serikali ya Jamhuri ya Muungano nchini Tanzania umewezesha kuwepo namna bora za kimaendeleo kwa wamachinga.
"Licha ya kufanya ujasiriamali katika hatua zetu leo hii tumeweza kupata mikopo ya kimaendeleo hatua inayochangia kukuza uchumi wa mmoja mmoja,"amesema Choga.
Amesema kuna hatua nyingine tofauti za zilizoanza awali kumlenga machinga kufikia maendeleo mengine kiuchumi ambapo vinakuja sasa vitambulisho vitavyoweza kuwa suluhisho katika maendeleo makubwa.
Ameongeza kuwa vinamfanano wa juu katika matumizi kwani namna za NIDA zitakuwa ndani na vipengele vingi vya muhimu vitavyoweza kutakiwa kwenye mifumo ya taasisi za kibenki vitakuwemo.
Tayari MAENDELEO BANK kwa ushirikiano mzuri na KAWASSO kwa kutambua juhudi za serikali ya awamu ya sita ya kumkwamua mwananchi kiuchumi ili kupunguza umaskini, walishaingiamakubaliano na chama cha wamachinga Kariakoo(KAWASSO) kwaajili ya kuwapa wamachinga mikopo ya gharama nafuu ya ununuzi wa viwanja pamoja na mkopo wa ujenzi wa nyumba za kisasa.
![]() |
| Kushoto ni kiongozi wa juu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum hivi karibuni wakiwa kwenye maongezi na Katibu KAWASSO Augustino Choga. |
Ambapo mbele ya waandishi wa Habari siku Mei 7,2024 wakati wa zoezi la utiaji wa saini mkataba wa ujenzi wa nyumba hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dkt Ibrahim Mwangalaba alisema Bank ilipokea maombi kutoka kwa KAWASO ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga ambapo walikubaliana kuanza ununuzi wa viwanja ambapo tayari wameshapata hekari 89 katika kijiji cha Magoza wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani

0 Comments