ORCHID ORGANIZATION IMEZINDUA BARCODE NA QR CODE KWA AJILI YA WAJASIRIAMALI.








 Taasisi ya Orchid organizations leo  tarehe 21February 2025mefanya  semina ya manunuzi ya umma kwa vikundi vya wajasiriamali, wanawake Na walemavu, kwa kushirikiana na PPRA jijini Dar es salaam na Vilevile Orchid organizations ilizindua Qr Connect, ambayo,Inahusisha Qr Code na Bracode ambapo wanapewa wajasiriamali wadogo wadogo,ambapo wanawawakaribisha wajasiriamali kujiunga na Orchid Organizations ili kupewa OR Code  na Bar Code,hata kama mjasiriamali ana bidhaa moja.

Ambapo kwenye uzinduzi huo  Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Lazaro Twange,alikuwa mgeni Rasmi na alisema kwamba"Hongereni sana Orchid organizations kwa kutatua baadhi ya Changamoto za wajasiriamali pia,nawasihi wajasiriamali kutafuta na kusoma vitu vizuri kama hivi kwenye mitandao ili iwasiaidie katika biashara zenu"

Pia Wengine waliohudhuria ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu Nasra Francis Pendo na Katibu wa Taasisi Lilian Mtundu  jana ubungo jijini Dar es salaam.

Naye Mkuu wa wilaya ya ubungo aliwapongeza Orchid organizations kwa kuzindua QR Code na Bar Code kwa jili ya bidhaa za wajasiriamali

Post a Comment

0 Comments