SHIGONGO: ‘’NCHI NI TAJIRI TUSIWE WANYONGE.”


Na Nancy Mawole 


Mbunge wa Buchosa na Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo, amewaasa watanzania kutokuwa wanyonge, bali wanapaswa kujivunia utajiri kupitia rasimali walizonazo. 


Amezungumza hayo leo Februari 22 akiwa na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya kurejea kutoka nchini Marekani ambako alikuwa kwenye ziara ya kikazi.


Mbunge huyo, alitoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuhakikisha Tanzania inajitegemea kiuchumi kwa kutumia rasilimali zake. Alisema kuwa mkakati wa kujitegemea utaifanya nchi kuendelea kwa kasi na kuwapatia wananchi fursa nyingi za maendeleo.


Katika hotuba yake, Shigongo alihimiza uzalendo na mshikamano miongoni mwa watanzania , akiwataka waamini katika uwezo wao wa kuleta mabadiliko chanya kupitia bidii na ubunifu.


Mkutano huo ulihudhuriwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.




Post a Comment

0 Comments