Na Nancy Mawole
BARAZA la madiwani laadhinisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti wa mwaka 2025/2026 ikiwa lengo ni kuongeza mapato ndani ya manispaa na kuwanufaisha wananchi kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Akizungumza katika Baraza hilo, Mwenyekiti wa kikao hicho Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Jaffary Nyaigesha amesema lengo la kikao hicho ni kujadili namna ya kuendelea kuwasidia wananchi katika kutatua changamoto zao katika maeneo mbalimbali ikiwemo afya, elimu, miundombinu.
Vilevile amesema kuwa kupitia mapendekezo ya mpango wa bajeti wametenga viwanja viwili vya michezo viwili katika wilaya hiyo lengo ni kukuza sekta hiyo na kukuza mapato ya ndani ya manispaa.
“Niwaambieni wajumbe wa Baraza jitihada zinaonekana twendeni tukatatue changamoto zilizosalia kwenye miradi ya kimaendeleo. Niwapongeze pia kwa ushirikiano mnaotoa katika kutoa huduma za kijamii kwa wananchi, “ alisema
Naye Mbunge wa Jimbo la Kibamba CCM Issa Mtemvu ameliomba Baraza kuweza kujenga soko la kimataifa katika wilaya hiyo ili kukuza uchumi wa nchi.
“ Serikali imekuwa ikipiga hatua katika kutatua changamoto mbalimbali na kwa sasa tunaweza kuona ujenzi wa nyota 5 katika kata Sinza umehusisha kwenye mapendekezo ya mpango wa Bajeti hii ni hatua kubwa
Hivyo basi itakuwa vyema tukihusisha jambo la ujenzi wa soko la kimataifa katika wilaya hii ikiwa katika rasimu ya mpango wa bajeti wa Mwaka 2025/2026,”amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Lazaro Twange ameahidi kushirikiana na Baraza katika kutatua changamoto mbalimbali katika wilaya hiyo.



0 Comments