MBUNGE SUBIRA MGALU: NISHATI SAFI YA KUPIKIA INALINDA AFYA ZA WANANCHI NA MAZINGIRA

 


Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Subira Mgalu, amesema makundi mbalimbali ya wajasiriamali, wakiwemo mama na baba lishe pamoja na wafanyabiashara wa Soko la Samaki Bagamoyo, yamenufaika na ugawaji wa mitungi 600 ya gesi ya kupikia uliotolewa na kampuni ya Oryx Gas wakati wa Tamasha la Samaki lililofanyika wilayani Bagamoyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Subira Mgalu alisema mpango huo unaunga mkono juhudi za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kulinda afya za wananchi, kuhifadhi mazingira na kupunguza matumizi ya nishati zisizo rafiki kwa mazingira.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Oryx Energies Tanzania, Imani Mtafya, alisema ugawaji wa mitungi hiyo ni sehemu ya mchango wa kampuni katika kuhamasisha matumizi ya gesi ya LPG nchini, huku ikiendelea kuwekeza katika miundombinu ya usambazaji wa nishati hiyo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga, amesema ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi unaendelea kuwa chachu ya kuwawezesha wananchi kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia, hatua inayochangia kuboresha afya, kulinda mazingira na kuinua ustawi wa jamii.

#SubiraMgalu #NishatiSafi #Bagamoyo #OryxGas #LPG #Nishati #Maendeleo #Mazingira #Tanzania #KiongoziOnlineTV

Post a Comment

0 Comments