Viongozi wa Serikali katika Mkoa wa Manyara katika wamechukua hatua kwa kuokoa maisha ya Mtoto Njiti ambapo kupitia Manyara Tanzanite Marathon Gala Dinner wamefakisha kukusanya jumla ya shilingi bilioni 1, 356,900,000 iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar Es Salaam
Akitangaza matokeo ya harambe hiyo, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Babati Vijijini, Mhe. Daniel Baran Sillo, amawashukuru watu wote walioshiriki katika zoezi hilo sambamba na kuwakaribisha katika mbio hizo zitakazofanyika mkoani Manyara.
Aidha, Naibu Spika, Mhe. Daniel Baran Sillo pamoja na Wabunge wa Mkoa Manyara, familia na marafiki zake wamechangia jumla ya shilingi milioni 26 katika Gala Dinner ya kufanikisha Manyara Tanzanite Marathon
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga amesema kuwa Manyara Tanzanite Marathon 2026 inatagemea kukusanya fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwenye mwendelezo wa kuelekea tarehe 22 Agosti 2026, ambapo ndiyo kilele cha Marathon yenyewe
Namba ya kuchangia #ManyaraTanzaniteMarathon
⏺ CRDB LIPA NAMBA: 113069180
⏺CRDB ACCOUNT 10401215064

0 Comments