Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Februari 09, 2026, amefanya ziara ya heshima nyumbani kwa Mzee Pius Msekwa, ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyejulikana kwa mchango wake mkubwa katika siasa na utumishi wa umma.
Ziara hii, iliyofanyika katika Wilaya ya Ukerewe, ni sehemu ya ziara ya kazi ya Mhe. Mtanda. Katika ziara hiyo, viongozi hao walizungumza masuala mbalimbali ya kijamii, lakini hasa afya na ustawi wa mzee Msekwa, ambaye ni mmoja wa wastaafu waliotumika kwa muda mrefu katika nafasi za juu za uongozi nchini.


0 Comments