HAMAD RASHID AMLILIA MREMA, AMTAJA KAMA MWANASIASA WA MFANO KUTOKEA

 





Na Teophil Mbunda Dar es Salaam

Mwenyekiti wa chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed  hii leo ametuma salamu za rambirambi kwa familia na chama cha TLP kufuatia kifo cha Mwanasiasa Mkongwe nchini, na Mwenyekiti wa Chama cha hicho 


Ameyasema alipokuwa akizungumza ba  waandishi wa habari kwenye Ofisi za chama hicho alipokuwa akifunguwa wiki ya kusherehekea  miaka kumi toka kuanzishwa kwa  chama cha ADC mwaka 2012

Augustino Lyatonga Mrema (77) ambae amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.


Pole hiyo ameitoa leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa wiki ya miaka kumi ya chama hicho, ambapo amewataka watanzania kumuenzi Mheshimiwa 

mrema kwani alikuwa na uwezo mkubwa katika masuala mbalimbali ya kisiasa 



Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo Jumapili Agosti 21,2022 saa 12: 15.


"Alikuwa kiongozi ambaye ni nguli kwa siasa zetu za Tanzania, amepambana katika chaguzi mbalimbali na za vyama vingi vya siasa, Nitamkumbuka kwa mchango wake kwenye siasa za chama kimoja hadi vyama vingi. Pia 


natoa Pole kwa familia na wana TLP. tuendelee kumuombea " Amesema Hamad Rashid Mohamed


Historia fupi ya nguli wa siasa nchini Hayati Mrema alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro, amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, pia mgombea Urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa 


mwaka 1995 ambao umekuwa ni uchaguzi wenye historia kubwa sana nchini kutokana na kuungwa mkono na Watanzania wengi na Baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere, baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha 


Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wakwanza wa vyama vingi.


Pia amewahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole



Post a Comment

0 Comments