DAWASA YAWAHAKIKISHIA MAJI YA UHAKIKA WAKAZI WA DAR ES SALAAM

 

                      Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Eng Cyprian John Luhemeja 


Dawasa yajipanga kuhakikisha Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani yanapata maji ya kutosha na uhakika, ili kuhakikisha inaendelea kuwa salama kupitia mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere Rufiji ambao upo katika hatua za mwisho kukamilika ujenzi wake.


Ameyasema  hayo Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Eng. Cyprian John Luhemeja katika Mkutano wake na Waandishi wa habari Makao makuu ya DAWASA yaliyopo Kinondoni, Mwananyamala, Dar es Salaam.


Aidha  Eng Luhemeja amesema kuwa mpaka sasa Mhandisi Mshauri yupo katika eneo la mradi anafanya ubunifu wa Bomba kutoka Mloka mpaka Kisarawe na Mloka mpaka Zanzibar kutakuwa na uwezo wa kusafirisha Lita zaidi ya Milioni 756 kwa siku .


"Katika hii miaka mitatu ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan Dar es Salaam itakuwa na mji mengi sana na itakuwa safi na salama kwa upande wa maji"amesema Eng Luhemeja.


Aidha Eng Luhemeja amesema katika mwaka wa fedha ujao 2023-2024 wanaendakujenga matanki 24 ambayo yatajengwa katika maeneo mbalimbali badala ya kutoa maji moja kwa moja kwenye mradi yatatolewa kwenye matanki baada ya kupampu maji na kujaza kwenye matanki.


"Tupo zaidi ya asilimia 80 tunahama kutoka analojia kwenda dijitali tunakwenda kuwa na mfumo wa scana mpaka sasahivi tumeshapata mkandarasi keaajili ya kujenga zoni na baada ya kujenga tutafunga kamera tunaanza na Ubungo pamoja na Kinondoni "amesema Eng Luhemeja.


Sanjari na hayo Eng Luhemeja amesema ndani ya miaka miwili ijayo watakuwa na mfumo wao wa jufatilia maji hiyo yote ni mipango ambayo inalengo la kupunguza tatizo la maji.


"Tunakwenda vizuri na hiyo ndiyo mipango ambayo tumeiweka ambapo tumepanga ikamilike kabla ya kuisha kwa awamu ya Kwanza ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan "amesema Eng Luhemeja.




                                       https://youtu.be/OXbbDBRjacg

Post a Comment

0 Comments