Makalla ametuma salamu kwa Bashiru ‘Kelele za kina Bashiru ni Kiranga’

 



                           Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, AMos Makalla


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla ametuma salamu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge, Dkt. Bashiru Ally baada ya kusema kuwa ‘Kelele za kina Bashiru ni Kiranga’ na wataendelea kumshukuru Rais Samia kwa kazi anayoifanya.


RC Makalla ameyasema hayo leo Novemba 25 katika ziara ya kukagua chanzo cha maji cha Ruvu chini na amemshukuru Rais Samia kwa kutoa Fedha zaidi ya Bilioni 300 kwaajili ya Ujenzi wa Bwawa la Kidunda ambapo amesema kuwa Bwawa hilo litahifadhi maji ambayo yatasaidia wakati wa ukame katika mikoa ya Dar Es Salaam na Pwani

"Tunamshukuru Mhe. Rais kwani Tunakwenda kukabiliana na Tatizo la mabadiliko ya Tabia nchi kwa sababu inapotokea Mvua zimechelewa Bwawa la Kidunda litasaidia kuhifadhi maji ambapo wakati wa ukame maji yatafunguliwa na tutaendelea kupata Maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani."

"Sisi Tutaendelea kushukuru na ndio Utamaduni wetu, kwahiyo hizo kelele kelele hizo za Akina Dkt. Bashiru mimi nasema ni kiranga Tupo 'Site' akate simu tunaendelea na Kazi, Tutaendelea kushukuru huo ndo utamaduni wetu."

"Mtu asiyetaka kushukuru kama yeye ana nyongo yake ya chuki ale ndimu ili kuondoa nyongo , Sisi tupo 'Site' Tutaendelea kufanya kazi na kutangaza mazuri anayofanya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan." - RC Makalla

Post a Comment

0 Comments