Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imewasilisha taarifa yake kuhusu mahojiano iliyofanya na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) huku Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda akikana kauli yake.
Akiwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati, leo Jumatatu Novemba 7, 2022, Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mussa Sima amesema kikubwa walichobaini ni mawasiliano hafifu.
Sima amesema kamati hiyo iliwaita HESLB Ijumaa iliyopita baada ya kuzungumza na waziri, naibu na katibu mkuu ambao hawakuonyesha shaka yoyote kuhusu utendaji wa bodi.
Kwenye taarifa hiyo ambayo ilikuwa na mapendekezo ya maazimio mawili, kamati imesema kauli iliyotolewa na Profesa Mkenda ndani ya Bunge haikuwa na uhalisia kwenye mazungumbo baina ya kamati na bodi hayakiwa na uhakika.
Akichangia ndani ya Bunge, Profesa Mkenda amekanusha hajawahi kulalamika ndani ya Bunge kwa kuwa anaimudu kamati hiyo.
Profesa Mkenda amesema pia hajawahi kusema kama bodi inamkwamisha kauli ambayo iliwaibua baadhi ya wabunge kumuombea mwongozo.
0 Comments