Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema atalipa msukumo somo lenye kombinesheni ya kiarabu, ili lifundishwe kidato cha tano na cha sita kwa sababu litasaidia kuzalisha wataalam watakaokwenda kukalimani kiarabu na kiswahili kwa kuwa ni lugha kubwa inayotumika umoja wa mataifa.
Ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam, wakati wa Mahafali ya Shule za Kiislamu za Ilala Dar es Salaam, yaliyofanyika katika uwanja wa Garden amesema somo la dini lipo kwenye mjadala ikiwamo masuala muhimu ya kuzingatia.
Aidha amesema kuwa, jamii haiwezi kukwepa suala la malezi bora kielimu na kimaadili hivyo ni wajibu wa walimu na wenye shule, kuhakikisha kuwa watoto wanapata malezi ambayo wazazi wanataraji ikiwamo kuwapo maadili mema.
0 Comments