KILO 2584.55 ZA DAWA ZA KULEVYA ZATEKETEZWA JIJINI DAR ES SALAAM




Muwakilishi wa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya  Veronica Matikila katika zoezi la uteketezaji wa dawa hizo uliofanyika




Na Magreth Mbinga 


Mamlaka ya  ya kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya imefanya zoezi la kuteketeza Kilo 2584.55 ya dawa za kulevya zikiwa katika mchanganuo tofauti tofauti.


Hayo yamezungumzwa na Muwakilishi wa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya  Veronica Matikila katika zoezi la uteketezaji wa dawa hizo uliofanyika katika kiwanda cha Thaluji cha Twiga kilichopo Wazo hill Jijini Dar es Salaam.


"Kilo 569 ni dawa ambazo tunaziita hard drugs kama vile Cocain na heroin,Tani 2 dawa aina ya bangi uteketezaji huu huwa unafanyika baada ya mashauri ya dawa za kulevya kuwa umeshakamilika mahakmani"amesema Matikila.


Pia Matikila amesema Dawa hizo za kulevya ambazo zinteketezwa Leo zinatoka katika Mahakama tofauti kama vile Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam,Mahakama kuu divisheni ya uhujumu uchumi pamoja na rushwa , Mahakama ya Akimu Mkazi Kisutu,Mahakama ya Akimu Mkazi Pwani na Mahakama za Wilaya.


"Zoezi hili kama mtakumbuka ni mara ya pili kufanyika ambapo mara ya kwanza lilifanyika mwanzoni mwa mwezi Disemba ambapo tulifanya katika Mikoa ya Kusini ambapo tuliteketeza jumla ya kilo 250 iliteketezwa katika kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara"amesema Matikila.


Aidha Matikila amesema mwaka 2021 waliteketeza jumla ya kilo 355 za dawa za kulevya aina ya metha tangu kuanzishwa kwa mamlaka ya kupambana na kudhibiti dawa za kulevya mwaka 2017 imekuwa ni mara ya tatu kufanya uteketezaji wa aina hiyo katika kiwanda hiko Cha Twiga.


"Kwa mara ya kwanza zoezi lilifanyika Oktoba 8 ,2019 ambapo kilo 120 za heroin na kilo 70 za cocaine ziliteketezwa ,mara ya pili tulifanya uteketezaji Novemba 12,2020 jumla ya kilo 119 za heroin na kilo 4 za cocaine na kilo 120 za bangi ziliteketezwa "amesema Matikila.


Sanjari na hayo Matikila amesema zoezi hilo la uteketezaji lipo kwa mujibu wa sheria kwasababu kama wanafanya mashauri na lengo lao ni kuhakikisha kwamba dawa hizo haziingii mtaani wanajukumu la kuhakikisha zinateketeza katika mazingira ambayo yatakuwa ni Salama kwa mazingira lakini pia hata wanadamu na viumbe hai .

Post a Comment

0 Comments