Makamu Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam Yusuph Namoto amesema mikopo inayotolewa na Benki ya Maendeleo Banki umekuwa na tija ya kuinua uchumi kwa wamachinga.
Namoto amesema wamefanikiwa kuufunga mwaka huu kwa manufaa baada ya benki hiyo kutoa mikopo kwa wamachinga 1800 ikiwa na riba nafuu.
"Maendeleo Benki imekua ikitupatia mikopo kwa waitaji hadi kufikia Wamachinga 1800 kwa mwaka huu na kusababisha kuinua uchumi wa kila mmoja," anasema Namoto.
Namoto alisema kuwa mikopo hiyo ililenga kwa wamachinga waliopo katika maeneo sahii waliopangiwa .
Pia Kiongozi huyo alipambanua kuwa jumla ya wamachinga wakiume waliopata mikopo hiyo ni 1244 na walifurahia uchumi wao kukua baada ya kuwezeshwa.
Makamu huyo Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam aliendelea kupambanua kuwa jumla nyingine iliyobaki waliopewa mikopo hiyo ni wanawake.
Aidha wamachinga hao ambao wanafunga mwaka kwa kuwa na tabasamu njema , utaratibu wa uongozi huo jijini hapa umeeleza kuwa mikopo hiyo inayoendelea kutolewa na benki hiyo ulianzia kiwango cha shilingi laki 3 .
Uongozi huo wa Machinga umeeleza kuwa mikopo yote inayoendelea kukopeshwa kwa mtu mmoja mmoja muda wa kurudisha mkopo ni wa miezi 6 mara kuanzia tarehe ya mkopo hadi utakapo rudishwa.
Baadhi ya maeneo yaliyofikiwa na mikopo hiyo ni Solo la Kariakoo ,Machinga Complex, Soko la Bog Brother, Solo la Feli, Maeneo ya Tabata Muslim .
Maeneo mwengine ni Tazara Vetenal ambapo imetajiwa kuwa kila mmoja aliyepata mkopo huo pia alikuwa tayari amekata Bima ya kujilinda na manjanga endapo itatokea ajali ya moto katika bidhaa zake nk.
0 Comments