KAMPUNI ya Mafuta ya Puma imeungana na Wanawake wote nchini katika kusheherekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika Machi 8 kila mwaka kwa kutoa zawadi ya Mafuta, na mitungi ya gesi ya kilo sita kwa wanawake wenye ulemavu ambao wanajishughulisha na uendeshaji wa bajaji za kusafirisha abiria.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Fatma Abdallah amesema siku ya Leo ya kipekee Kidunia wamefanya hivyo kwa kutambua nafasi ya mwanawake katika Jamii kwani hao wenye ulemavu wanaofanya shughuli hizo katika jiji la Dar es Salaam kujipatia kipato kuepuka utegemezi.
Hata hivyo amesema Kampuni ya Puma imeona kuna kila sababu ya kuungana na wanawake hao kuadhimisha siku hiyo lengo likiwa ni kutambua mchango wao sambamba na kuwapa moyo kwamba Ulemavu walionao sio sababu ya kuwa wanyonge kutofanya kazi na kuwa tegemezi katika jamii.
“Kampuni ya Mafuta ya Puma tunajihusisha na biashara ya uuzaji Mafuta, vilainishi, pamoja na nishati safi ya gesi ya kupikia hivyo Siku ya leo tumeamua kutoa zawadi kwa kuwajazia Mafuta wanawake wenye Ulemavu ambao wanatoa huduma ya kusafirisha abiria katika Jiji la Dar es Salaam.
"Pia mbali na kujaza Mafuta full tank tunawapa na zawadi ya mtungi wa gesi kila mmoja tunataka wanapofanya shughuli zao wasifikirie kuchelewa kuandaa chakula kwa jiko gani,” amesema Fatma na kuongeza,
“Lakini kutoa zawadi ya mitungi ya gesi kwa wanawake hawa wenye ulemavu ni kitumia siku hii kuungana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha nishati safi ya kupikia na kuachana na kuni na mkaa, hivyo pamoja na mambo mengine tunatumia siku hii ya wanawake duniani kihamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia,”.
Kwa upande wake Sophia Abdallah dereva bajaji mmoja wa wanufaika wa zawadi hizo, ameishukuru Kampuni ya Mafuta Puma kwa kiwajazia mafuta full tank na kuwapatia mitungi ya gesi ya kipikia.
Sanjari na hayo mewahamasisha akina mama nchini kutumia Nishati ya gesi mbadala ya Kampuni hiyo kwani unaweza kuagiza kwa njia ya mtandao popote uliopo na ukaketewa kwa kiasi cha fedha unachohitaji ni gharama nafuu pia


0 Comments