Na: Mwandishi Wetu Dar es Salaam
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimewakaribisha wanafunzi waliomaliza elimu ya sekondari mwaka huu na kupata alama ambazo zinakidhi kujiunga na vyuo vikuu kujiunga na chuo hicho ili kupata elimu itakayo wawezesha kujiajili katika sekta mbalimbali.
Akizungumzia kwenye maonesho ya vyuo vikuu yanayoandaliwa na TCU kwenye banda la Chuo mara baada ha ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 18 Jijini Dar es salaam Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Lughano Kusiluka amewakaribisha watu wote kutembelea katika banda lao na kupata taarifa mbalimbali kuhusu UDOM pia kuweza kupata fomu za kujiunga na chuo hicho.
"Tumekuja hapa kwa ajili ya kuwaelimisha wale wanaotaka kujiunga na Chuo namna ya kuingia kwenye mfumo wa kujisajili na kujiunga na kuweza kuchagua program ambazo mtu unazihitaji na tunao wataalamu kwenye Banda hili kubwa kuliko mabanda yote katika maonyesho haya na hiyo inatafsiri ukubwa wa UDOM" Alisema Prof Kusiluka
Alisema wananchi, wahitimu na hata watu binafsi ambao wanatamani kujiendeleza na masomo ya fani mbalimbali kufika katika banda lao kwa ajili kupewa maelezo kwa sababu hakuna fani ambayo inafundishwa katika nchi hii kwasasa ambayo huwezi kuipata katika Chuo hicho.
Alisema Tunawatayarisha vijana wetu kwaajili ya kujiajili baada ya kumaliza masomo yao, wote tunajua kwamba fursa za ajila sio nyingi lakini mara baada ya kuhitimu chuo hapo utaweza kutengeneza fursa za ajila kwa ajili yako mwenyewe lakini na kwa ajili ya watu wengine.

Profesa Kusiluka ameongeza kuwa kupitia maonyesho hayo pia wanatoa taarifa mbalimbali ikiwemo kuhusu utafiti, machapisho na maendeleo ya teknolojia sasa hivi mnasikia kuhusu Artificial intelligence (Akili mnembo) imefika mahali inaanza kutuchanganya ila pale UDOM tunaowataalamu na siku za hivi karibu tutaanza kutoa kozi fupi ili watanzania waweze kuijua Akili bandia ambayo inatikisa Dunia kimaendeleo badala ya kuteseka nayo tujitayarishe kuitumia kwasababu imetukuta na sisi hatuwezi kuikimbia.
Aidha amebainisha kuwa UDOM imekuwa ikifanya vizuri katika maeneo mbalimbali hususani katika Tehama na Sheria ambapo wamekuwa washindi katika Mashindano mbalimbali Barani Afrika.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Lughano Kusiluka akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi waliopo katika maonyesho hayo ya Maonyesho ya 18 ya Elimu ya juu, sayansi na teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja Jiji Dar es salaam

0 Comments