Na Magrethy Katengu
Kampuni ya Uwekezaji UTT AMIS imeendelea kuleta kwa kwa kufikia kiasi cha fedha TSH Trillion 1.5 ukuaji huo sawa na asilimia 54 kwa mwaka 2023 ukilinganisha na mwaka juzi ukuaji wa taasisi kutoka Sh bilioni 600 hadi Sh bilioni 996 sawa na asilimia 50 kwa mwaka 2022 kutoka Sh bilioni 996 ukuaji huo mfuko haujawahi kuyumba wala kushindwa kujiendesha
Ameyasena hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa UTT AMIS Simoni Migangala Jijini Dar es Salaam katika semina fupi iliyoandaliwa na ofisi ya Msajili wa Hazina na Jukwaa la Wahariri (TEFF) pamoja na Waandishi wa habari lengo ni kuwaelimisha namna Mfuko wa UTT AMIS Mafanikio yake na unavyosaidi wananchi kuweza fedha zao ili kujikwamua na umasikini
"Tunashukuru Wananchi umekuwa na mwitikio mkubwa kwa Watanzania kujitokeza kuwekeza na mifuko inayoendeshwa na iliyo chini ya kampuni ikiwemo Mfuko wa umoja,wekeza maisha,mfuko wa mtoto,mfuko wa kujikimu,mfuko wa ukwasi,mfuko wa hati fungani ambapo ukuaji wa thamani ya uwekezajin(Vipande) na mtu kuanzia umri wa mika 18 anaanza kuwekeza na hupata fedha zake pale anapozihitaji kama akipatwa na dharura"amesema Mkurugenzi.
Sanjari na hayo amefafanua kuhusu mafanikio ya miaka minne mfululizo waliopata kutokana na uwekezaji mdogo na mkubwa ambapo ilikuwa kwa mwaka juzi ukuaji wa taasisi kutoka Sh bilioni 600 hadi Sh bilioni 996 sawa na asilimia 50 kwa mwaka 2022 kutoka Sh bilioni 996 hadi Sh Trilioni 1. 5 sawa na asilimia 54 ukuaji huu umeenda vizuri ikilinganishwa na kipindi cha nyuma, na kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni, mwaka huu ukuaji umeongezeka kwa asilimia 12 na kwa miaka sita wakitoa gawio serikali.
Naye, Mkurugenzi wa Masoko UTT Amis, Daud Mbaga amesema Hapo awali ilimbidi mwekezaji wetu aende benki moja kwa moja ili kununua vipande, lakini kwasasa Mwekezaji anaweza kununua vipande kupitia njia zote za malipo za benki ya CRDB yaani Simbanking, CRDB App na Fahari Huduma.u
"Tumia simu yako ya mkononi huduma za Tigopesa, Airtel Money, M-Pesa, T-pesa na Halopesa inawezekana kununua vipande kwa kutumia program tumizi (App) za benki ya Amana na Standard Charter mwekezaji unaweza kununua vipande moja kwa moja kwani teknolojia imekuwa na kusaidia kuwafikia na kuwahudumia wawekezaji wetu kwa urahisi,” amesema.Daudi
Mbaga, ameongeza kuwa katika kufanikisha UTT AMIS, inaendelea kupiga hatua wamekuwa wakitoa elimu ya uwekezaji katika ngazi mbalimbali ikiwemo vyuoni na sasa wana mkakati wa kuhakikisha kuwa kwenye mitaala ya elimu linaongezwa somo hilo.
“Kwa sasa, UTT AMIS ndio habari ya mjini kutokana na wawekezaji kujitokeza kwa wingi kwetu na kipindi cha Covd kwetu kilikuwa ni kizuri kutokana na watu walikuwa wakiwekeza kwetu na kilitupa mafanikio,” amesema








0 Comments