BODI YA SUKARI YATOA RAI KWA WAFANYABIASHARA WANAOUZA BEI KIHOLELA

 



Na: Sheila Ahmadi

Bodi ya Sukari Tanzania imewataka wafanyabiashara wote  nchini ambao  wanauza bei ya sukari isiyo halali kuacha mara moja kwani  serikali ya awamu ya sita inaenda kuchukua   hatua kali za kisheria dhidi  yao  na ambao.wataendelea kuwauzia wananchi  bei  holela.

Hayo  yamesemwa  jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Profesa Kenethy Bengesi , ambapo wamebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara ambao siyo waaminifu nchini wanauza sukari kwa bei isiyo halali wakati wananunua kwa bei ya kawaida hivyo na kuwafanya Watanzania kuishi kushindwa kumudu gharama za bidhaa hiyo muhimu.

”Bodi inatambua kuwa kila mkoa unatofautiana bei ya sukari hivyo wafanyabiashara wanaopandisha bei kwa maslahi yao binafsi tofafauti na bei halali ya mkoa huo tukiwabaini hatutawaacha tutahakikisha tuwachukulia hatua kali za kisheria kwani hatupendi kuona wananchi wakilalamika juu ya bidhaa hii muhimu kupandishiwa bei holela” amesisitiza mkurugenzi.

uhaba wa sukari uliopo kwa  sasa    imetokana na kunyesha  kwa  mvua za El nino zilizoanza Oktoba 2023 na kupelekea mashamba ya miwa kujaaa maji pamoja na miundombinu ya barabara kuharibika hivyo kushindwa kuvuna miwa iliyotakiwa kupelekwa kiwandani kuchakatwa kwa  sukari .

”Mwaka huu tumezalisha tani 345,000 pekee ambazo hazitoshelezi lakini kawaida mahitaji huwa ni tani 520,000 na katika uzalishaji tunapenda malengo yetu ni kuzalisha tani laki tano na hamsini na tano ili tuwe na akiba ya sukari ya kutosha lakini kutokana Msimu huu wa mvua za El nino tumeshindwa kufikia lengo ndiyo maaana tuna uhaba wa sukari” amesema Bengesi.

Sambamba  na hayo  profesa  mangesi amebainisha kuwa   Serikali imechukua hatua za kukabiliana na uhaba wa sukari kwa kutoa kibali kwa kuagiza sukari nje ya nchi tani 50,0000 na kwama sukari hiyo inatarajiwa kuingia nchini Januari 22 , 2024 .

Kutokana na changamoto hizo  serikali  inaenda kuhakikisha suala hilo la sukari  linaenda kutoweka kwani ni huduma muhimu hususani kw mama ntilie

Wanakosa huduma hiyo kwa sababu ya bei ambazo zinaendelea nchini hivyo  bodi  ya sukari imejipanga vyema katika kuwainua wananchi nchini kwenye suala la sukari.




Post a Comment

0 Comments